Mwanachama wa klabu ya Yanga na mpenzi maarufu wa soka nchini, Ally Mohamed anayejulikana zaidi kwa jina la utani ëAlly Yangaí amefariki dunia leo baada ya ajali ya gari iliyotokea, eneo la Mpwapwa, Dodoma.
Taarifa zinasema Ally Yanga alikuwa kwenye msafara wa mbio za Mwenge kabla ya kupata ajali hiyo barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipogoro na kufariki hapo hapo.
Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.
Aliibukia Ubungo miaka ya nyuma kidogo ambako alikuwa anafanya shughuli ya kusajili laini za simu za mkononi katika vibanda vilivyokuwa pembeni ya kituo kikuu cha mabasi ya mikoani, Ubungo Terminal.
Na alianza kuonekana Uwanja wa Taifa pamoja na kikundi cha mashabiki wa Yanga cha Ubungo Terminal, ambako ndipo lilipokuwa tawi lake,Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.
Ally hakuwa shabiki wa Yanga tu, enzi za uhai wake alikuwa akizishabiki pia timu za taifa, kuanzia za vijana na wakubwa za wanawake na wanaume, jambo ambalo lilimpa umaaarufu zaidi kwa kupeda mchezo wa soka.
Alikuwa maarufu Afrika Mashariki kutokana na kwenda kuishabikia Taifa Stars kwenye mechi za Kombe la CECAFA Challenge nchi za Kenya na Uganda. Lakini pia amewahi kusafiri hadi nje ya Afrika ya Afrika Mashariki akiwa na Taifa Stars kwenye mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika na Kombe ka Dunia.
No comments:
Post a Comment