Wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania akiwemo
msanii mkongwe katika soko la muziki Juma Kasim maarufu kama Juma
Nature, Msanii mkongwe wa Muziki wa taarabu Khadija Omar Abdallah Kopa
maarufu kama Malkia wa Mipasho, Band ya Twanga Pepeta sambamba na
wasanii wengine zaidi ya kumi wametumbuiza kwenye sherehe za Mkesha Wa
Mwenge wa Uhuru 2017 zilizofanyika usiku wa kuamkia Leo Tarehe 1, Juni
2017 katika Viwanja Vya Barafu, Manispaaya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Katika
Sheree hizo zilizoratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare
Makori kwa ushirikiano Mkubwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg
John Lipesi Kayombo sambamba na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg
James Mkumbo wananchi waliitikia wito kwa kujitokeza kwa wingi Jambo
ambalo limeimarisha umahiri wa Mwenge wa Uhuru ambao kwa mwaka huu una
kauli mbiu isemayo Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya
nchi yetu.
Pamoja na kauli mbiu ya kutilia msisitizo
kuhusu uchumi was viwanda pia Mwenge was Uhuru umebeba jumbe mbalimbali
ikiwemo kupiga Vita Maambukizi mapya ya UKIMWI na Malaria sambamba na
kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Awali
kabla ya mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika Viwanja hivyo vya
Barafu-Mburahati Mwenge huo ulizuru katika miradi mitano katika Manispaa
hiyo Kama ifuatavyo;
1. Uzinduzi wa
Jengo la Kituo Cha Huduma kwa wagonjwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi
(VVU) katika kituo Cha afya Mbezi. Jengo hilo limegharimu kiasi cha Tshs
125 milioni ambazo zimetolewa na wafadhili ambao ni MDH (Management
and Development for Health).
2. Kuweka
Jiwe la Msingi wa Kituo Cha Polisi Cha Kati-Kata ya Kibamba ambapo
wananchi wamekwisha changia jumla ya Tsh. 53,000,000/ = huku NSSF
ikichangia Tsh. 50,000,000/= sawa na jumla ya Tsh. 103,000,000/=
3.
Uzinduzi wa madarasa nane katika Shule ya Msingi Malambamawili Kata ya
Msigani, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam. Jengo hilo lenye
madarasa nane (8) yaliyozinduliwa yamejengwa kwa fedha kutoka Serikali
kuu kwa gharama ya Shilingi Milioni mia moja na thelethini na sita
(Tshs 136,000,000/=)., madarasa hayo Yakikamilika shule itakuwa na
vyumba vya madarasa 24.
4. Uzinduzi wa
Mradi wa Mabasi SIMU 2000 Uliopo katika Kata ya Sinza. Kituo hicho
kimejengwa kwa kutumia fedha zilizotokana na Mapato ya Ndani (Own
Source) Gharama yake ni Shilingi 2,376,647,991.89 chini ya Mkandarasi
M/S DEL MONTE (T) LTD.
5. Mradi wa
Ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Mburahati katika eneo la Mtaa wa NHC Kata
ya Mburahati. Mradi huu wa ujenzi wa zahanati ulianza kutekelezwa
tangu Juni 2014 na kukamilika mnamo Oktoba 2016 chini ya Manispaa ya
Ubungo, kwa gharama ya kiasi cha Tshs 84,000,000.00.
Tayari
Mwenge wa Uhuru umekwisha ondoka Katika Mkoa wa Dar es sala ambapo Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amemkabidhi Mkuu wa Mkoa
wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano
iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere
Terminal 1 tayari kwa kuelekea Mafia Mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment