BREAKING

Monday 29 February 2016

SHULE 18 DAR KUNUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUTOKA KWA CFAO MOTORS GROUP NA ALLIANCE AUTOS

IMG_4204
Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin, (katikati)  na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school, Henning Nathow.
Katika kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Akizungumzia msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao wengi wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka barabara.
Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha alama za kusimamisha magari ili wanafunzi wavuke, makoti yanayowatambulisha waongozaji, kofia za kuwazuia na jua na mipira ya michezo mashuleni na watatoa elimu katika shule hizo ili kuwasaidia watoto kujua sheria za barabarani.
“Tumeamua kutoa msaada huu kwa shule 18 na tutatoa elimu na tutakabidhi vifaa … tunaamini msaada huu utaweza kuwasaidia watoto hao na tunaamini itasaidia kupunguza ajali barabarani,” alisema Bi. Tharaia.
Akipokea vifaa hiyvo kwa niaba ya Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter alisema wanaishukuru CFAO Motors Group kwa kutambua umuhimu wa elimu na kutoa vifaa vitakavyoweza kusaidia kuongoza wanafunzi wavukapo barabara.
“Tunashukuru sana kwa msaada huu na mmeonyesha ni jinsi gani mnatambua umuhimu wa elimu na sisi tupo pamoja nanyi na tupo tayari kupokea elimu hiyo,” alisema Bi. Helen.
Alizitaja baadhi ya shule ambazo zitapata vifaa hivyo kuwa ni Shule ya Msingi Msimbazi, Boma, Mnazi Mmoja, Uhuru Mchanganyiko, Tabata, Ilala, Lumumba, Muhimbili, Buguruni, Kasulu, Mkoani, Msimbazi Mseto, Hekima, Amana, Mtendeni, Buguruni Viziwi na Tabata Jeta na Mtandani.
Pamoja na hayo pia kunataraji kufanyika mashindano ya mbio za magari yaliyo na lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya CFAO Motors Group yanayofanyika nchini na yanataraji kumalizikia nchini Rwanda.
Attu Mynah
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah (kulia) akionyesha baadhi vifaa hivyo vya usalama barabarani kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mbio hizo za kusaidia elimu nchini Rwanda zimepewa jina la The go4school Charity Rally ambazo zimeshirikisha magari 18 ambayo yameanzia jijini Dar es Salaam na yanataraji kufikia kilele chake Machi, 13 nchini Rwanda na yatapita katika nchi za Kenya na Uganda na kisha Rwanda.
Akizungumzia mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin alisema mbio hizo za magari zimeanzishwa na taasisi ya Volkswagen kwa kushirikiana na taasisi ya Opportunity International Germany kwa kutambua kwao umuhimu wa elimu na usalama wa watoto wawapo barabarani.
Alisema kuwa wamekuwa wakisaidia zaidi katika sekta ya elimu na sio mara ya kwanza kufanya mbio hizo za magari kwani mwaka 2013 walifanya mbio kama hizo kutokea Senegal hadi Ghana na mwaka 2015 walifanya kutokea Namibia hadi Malawi na mara zote kampuni ya CFAO Motors Group imekuwa ikihusika kufanikisha mbio hizo.
Henning Nathow
Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya go4school, Henning Nathow (wa pili kushoto) akielezea dhumuni lengo lao la kusaidia upatikanaji wa elimu bora kupitia mradi wa go4school.
“Mbio hizi zimeanzishwa na Wajerumani ili kusaidia elimu ya Rwanda na hii sio mara ya kwanza tayari yamefanyika mara mbili barani Afrika  na sisi kama CFAO tumekubali kuungana na taasisi ya Opportunity International Germany ili kusaidia upatikanaji wa elimu,” alisema Potin.
Nae Henning Nathow ambaye ndiyo mwanzilishi wa mradi wa go4school ulio na lengo la kusaidia upatikanaji wa elimu bora alisema wanafurahi kufanya mbiao hizo ambazo zina lengo la kusaidia elimu nchini Rwanda wa wanaamini elimu ndiyo njia pekee inayoweza kusaidia kupambana na umasikini.
Alisema wanataraji kufanya mbio hizo na baada ya kufika Rwanda watayakabidhi magari yanayotumika kwa ofisi za CFAO za Rwanda na baada ya hapo watayauza na mapato yatakayopatikana watayakabidhi kwa serikali ya Rwanda ili kusaidia sekta ya elimu.
“Elimu ni njia ambayo inaweza kusaidia kumaliza janga la umasikini na sisi tuna furaha kufanya mbio hizo kuelekea Rwanda ili kusaidia kupatikana kwa elimu bora Rwanda,” alisema Nathow.
Helen Peter
Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya CFAO Motors Group kwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilipo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Eric Potin
Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin (wa pili kushoto) akimkabidhi Afisa Elimu ya Ufundi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Helen Peter (wa kwanza kushoto) msaada wa vifaa vya usalama barabarani kusaidia wanafunzi wavukapo barabarani pamoja na vifaa vya michezo, Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed na (kulia) na Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah.
Eric Potin
Attu Mynah
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

MAJALIWA APOKEA MISAADA WILAYANI RUANGWA

hal1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya HUAWEI ya China , kijijini hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa Mtalaam wa Ufundi wa Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, Tran The Hoang ili ziweze kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani humo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ma  Mwanaidi Mussa  na Mkussa Lukoloma (kushoto) wote wa kijiji cha Nandagala wilayani  Ruangwabaada ya kuwakabidhi kadi zao za bima ya Afya ambazo zimegharimiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel iliyochangia shilingi milioni tisa kuwawezesha wakazi wa kijiji hicho kufaidi huduma za Bima ya Afya, Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti  watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti  watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
hal7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sunday 28 February 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA. DK KIGWANGALLA AKUTANA NA WATAALAM WA MPANGO WA BRN WA WIZARA YAKE



DK KIGWANGALLAWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisikiliza mambo mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN). Katika mkutano huo leo Februari 27.2016, jijini Dar es Salaam.
DK hk7Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Kushoto) akisikiliza kwa umakini masuala mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN). Mkyano huo unafanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, leo Februari 27.2016.
dk hk 80Wajumbe wa BRN wa Wizara ya Afya wakitoa maelezo yao mbalimbali kwa Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
dk hk jjjaDK KIGWANGALLA BRN67Wajumbe wa BRN wa wizara ya Afya wakifuatilia kwa umakini mkutano huo na Naibu Waziri (hayupo pichani)
Naibu Waziri Dk.Kigwangalla akisikiliza kwa umakini pamoja na wajumbe wengine katika mkutrano huo ambao amekutana na wajumbe wa timu ya wataalam wa Wizara yake hiyo wanaoshughulikia masuala ya BRN.
dk kigwangalla BRNMjumbe wa Wizara hiyo anayeshughulikia mpango wa BRN, Bw. Benard Konga akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla katika mkutano huo
dk hkii
DK KIGWANGALLA2Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisikiliza mambo mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN).
dkk hk21Mkutano huo ukiendelea..
DK KIGWANGALLA6Wajumbe wa Wizara ya Afya wanaoshughulikia mpango wa BRN wakifanua jambo.
dk hk7wNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisikiliza mambo mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN).DK KIGWANGALLA BRN67Baadhi ya Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN) wakifuatilia mkutano huo mapema leo Februari 27.2016, katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Dk Kigwangalla BRN3 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisikiliza mambo mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN) katika kikao maalum alichokutana nacho mapema leo Februari 27.2016, katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es  salaam


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo Februari 27.2016 amekutana katika kikao maalum na Wataalam wa Wizara hiyo ambao wapo katika timu inayoshughulikia Mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN) katika kufanikisha namna ya utoaji huduma bora na ufanisi katika mipango mbalimbali ya kufikia malengo ambayo Serikali ya Tanzania ilianzisha mpangp huo.
Dk. Kgwangalla amekutana na wataalam hao kwa mara ya kwanza, ilikupata mrejesho na kuelewa kiundani namna Wizara yake inavyotekeleza mpango huo wa matokeo makubwa sasa (BRN).
Aidha, Sekta ya Afya ni ya nane (8), katika Sekta zinazotekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN).





WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MH. NAPE NNAUYE, ASHIRIKI MBIO ZA KILI MARATHON, KILIMANJARO






Thursday 25 February 2016

MPANGO WA PUSH FOR CHANGE KUWASAIDIA WAKULIMA KATIKA UPATIKANAJI WA HABARI ZA MASOKO NA MITAJI


Tazama video hapa:
push mobileMkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd, Bw. Freddie Manento akizungumza katika mkutano huo leo Feb 25.
push jjjWadau wa kilimo wakifuatilia mkutano huo ..
pushjMkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd, Bw. Freddie Manento akizungumza katika mkutano huo. Kulia kwake ni Profesa wa chuo cha Sheria, Arizona, Dale Beck Furnsh
push mobile3Ofisa mahusiano wa wateja wadogo na wa Kati kutoka benki ya CRDB, Bi. Rehema Shambwe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
 
Kongamano la siku tatu juu ya sera ya kilimo linalotarajia kufikia tamati leo Februari 25.2016 huku likiwa limeshirikisha wadau wa kilimo Zaidi ya 150, kutoka ndani ya nje ya Tanzania wametoa maoni yao mbalimbali namna ya kuboresha kilimo hapa nchini ilikufikia maendeleo makubwa.
Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu: “Mabadiliko ya sekta ya kilimo na mchango wake katika kukuza usalama wa chakula na lishe, kupunguza umasini na kuleta ajira’ limefanyika jijini Dar es Salaam ambapo wadau hao wameweza kutoa maoni yao hayo ikiwemo namna ya kufikia wakulima kwa njia teknolojia ya mawasiliano.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd, Bw. Freddie Manento amebainisha kuwa masuala ya teknolojia na mawasiliano yanarahisisha upatikanaji wa habari mbalimbali ikiwemo Kilimo ambapo kampuni yake imeamua kurahisha mpango huo ilikumfikia kila Mtanzania ikiwemo hata yule wa hali ya chini kupitia mawasiliano na fursa za kupata taarifa sahihi.
Amebainisha kuwa, wakulima wanahitaji kupatiwa taarifa muhimu mbalimbali hivyo wao wameweza kuboresha huduma za teknolojia ya kufikisha habari hizo kupitia mpango wa Push for Change, ambao Mkulima kupitia simu yake hata kama ni ya kawaida anaweza kupata habari za kina juu ya masoko na namna ya kuwezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika.
Progamu ya Push For Change inatoa taarifa mbalimbali hivyo kuwa msaada mkubwa kw sekta ya kilimo. Huduma hyo pia wakulima na watu wengine wanaweza kuipata kwa kujiunga na huduma hiyo, kwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kuchagua huduma unayotaka ikiwemo kupata taarifa kama Kilimo, Uchumi, biashara, afya, michezo na burudani, savei, elimu, utaliii na nyinginezo.
Aidha, kwa upande wake, Ofisa mahusiano wa wateja wadogo na wa Kati kutoka benki ya CRDB, Bi. Rehema Shambwe amebainisha kuwa wamekuwa wakitoa mikopo na ushauri kwa wakulima mbalimbali huku changamoto kubwa ni suala la mitaji kwa wengi wa wakulima hao.
Bi. Rehema Shambwe amewataka wadau na Serikali kuangalia namna ya kuweza kuboresha bidhaa zinazotoka Tanzania ilikuweza kuhimili masoko ya Kimataifa.


ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MIKOA YA MWANZA, GEITA NA KAGERA

● Aziagiza Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi ● Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu ● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao ● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya
mab01
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji wa Buchosa alipowasili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
MAB1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana. MAB2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt Medard Kalemani wakikagua eneo la Kijiji cha Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada ya eneo la ekari 500 la kupewa mwekezaji.
MAB4
Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera Bw. Deogratius Batakanwa akimpewa maelekezo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuhakikisha kuwa anatoa elimu ya kutosha itakayowezesha wananchi, taasisi na Halmashauri ya Muleba kukamilisha ununuzi wa nyumba zilizojengwa na NHC Wilayani Muleba.Naibu Waziri alitembelea nyumba hizo na kulipongeza Shirika la Nyumba kwa ujenzi wa nyumba bora.
MAB5
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Muleba baada ya kuhutubia Baraza lao na kuliomba liwezeshe ununuzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo. Pia aliagiza Baraza hilo kushiriki kikamilifu katika kutatua migogoro mingi ya ardhi iliyoko katika Wilaya hiyo.
MAB6
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akikagua nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Mkoani Geita kwa ajili ya kuuza. Amewataka wananchi na Halmashauri ya Mji wa Geita kununua nyumba hizo ili kuliwezesha Shirika kuendelea kujenga nyumba katika Halmashauri zingine.
MAB7
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Mabula akiwa na Mbunge wa Chato Mhe. Dkt Medard Kalemani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini wakikagua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Chato. Katika ziara hiyo Naibu Waziri ameishauri Halmashauri ya Chato kununua nyumba hizo ili NHC iongeze ujenzi wa nyumba zingine kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nyumba Wilayani humo.
MAB8
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za NHC Mkoa wa Kagera alipotembelea na kusalimiana na wafanyakazi wa Shirika hilo.
MAB9
Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza Injinia Benedict Kilimba akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita, kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula alipotembelea mradi huo. Mhe. Naibu Waziri ameziagiza Halmashauri nchini kusaidia uwekaji wa miundombinu kwenye maeneo ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na kutoa ardhi bure kwa NHC ili nyumba zinazojengwa ziwe na gharama nafuu kwa mnunuzi.
MAB10
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bibi Mwajuma Nyiruka akitoa taarifa ya sekta ya ardhi ya Wilaya yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula alipoitembelea Halmashauri ya Misungwi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
MAB11
Baraza la Madiwani Muleba wakimsikilza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula (hayuko pichani) alipohutubia Baraza hilo.

RAIS WA MAGUFULI ATEMBELEWA NA UGENI KUTOKA GUINEA BISSAU..







JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of ArmsKURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais waJamhuri ya Guinea Bissau Mheshimiwa Jose' Mario Vaz amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali, hususani katika uchumi kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.
Rais Jose' Mario Vaz amesema hayo katika ujumbe wa barua uliwasilishwa kwa Rais Magufuli na Mjumbe maalum wa Rais huyo Jenerali Omar Embalo, Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 25 Februari, 2016.
"Napenda kusisitiza kuwa nchi zetu ni marafiki wa muda mrefu, naomba urafiki na mahusiano haya mazuri yaendelee na ninakuhakikishia kuwa nchi yangu itaendelea kuuenzi ushirikiano huu" Ilieleza sehemu ya ujumbe huo.
Aidha, Rais Jose Mario Vaz amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano na amemualika kuitembelea nchi ya Guinea Bissau ili kuimarisha zaidi Uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais Jose Mario Vaz kwa kumtuma mjumbe maalum kwa ajili ya kumletea ujumbe wa pongezi, na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Guinea Bissau.
"Nakushukuru sana Jenerali Umaro Sissoco Embalo kwa kuniletea ujumbe wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau na nakuomba umwambie namshukuru kwa pongezi, mimi na serikali yangu tupo tayari kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Guinea Bissau ili mataifa yetu yaweze kunufaika zaidi"Alisema Rais Magufuli
Wakati huo huo, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Ikulu Jijini Dar es salaam leo.
Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Februari, 2016

BREAKING NEWS:SEMINA ELEKEZI KWA MAWAZIRI NA MANAIBU KWA HABARI ZAIDI BLOG YAKO ITAKULETEA HAPA



Mawaziri na Na Naibu Mawaziri wameanza kuwasili Ukumbini Tayari kwa Semina Elekezi.(Na Mpiga Picha wetu David Ramadhan )

Sehemu ya Ukumbi wa Semina
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube