BREAKING

Tuesday 11 July 2017

WAZIRI MWAKYEMBE ASITISHA UTEUZI WA MALINZI WA BMT NA WAJUMBE WOTE BMT



DK.HARRISON MWAKYEMBE-Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akizunggumza na wanahabari hawapo pichani, kutangaza kuengua safu ya Uongozi wa BMT

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, DK. Harrison Mwakyembe amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi pamoja na wajumbe wote wa baraza hilo.

Waziri Mwakyembe amechukua uamuzi huo leo Jumatatu katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kufuatia agizo la waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati wa hotuba yake ya kufunga bunge, kuvunjwa kwa BMT kama haitaonekana kuwa na utendaji mzuri.

Licha ya kusitisha uteuzi wa mwenyekiti wa baraza hilo waziri huyo pia amesitisha uteuzi wa wajumbe wote katika baraza hilo huku sekretarieti ikipewa jukumu la kuendelea na kazi zake kwa kushirikiana na serikali wakati ikijipanga kwa ajili kuanza mchakato wa kutafuta viongozi wapya.

Wakati Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wake Dk John Pombe Magufuli, wakati ikiingia madarakani ilieleza nia yake thabiti ya kuendeleza michezo na kufanya sehemu ya ajira kwa vijana hususani wenye vipaji vya michezo pamoja na kupunguza migogoro ambayo ilikuwa ikijitokeza mara kwa mara..

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube