BREAKING

Monday, 24 July 2017

MAOFISA UGANI WATAKIWA KUTUMIA MAFUNZO WANAYOPATA KUWAELIMISHA WAKULIMA


Mtafiti, Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akizungumza na maofisa ugani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa maofisa hao kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo Mkoani Tabora leo.



 Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo ya Uyui,  Deogratius Mwampinzi, akizungumza katika mafunzo hayo. Kushoto ni Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora, Said Babu.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora, Said Babu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
 Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru, mkoani  Mwanza, Bakar Japhet akitoa mada.

Mtafiti wa pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru, mkoani  Mwanza, Stellah Chilimi akitoa mada.
 Maofisa Ugani wa wilaya hiyo wakiwa katika mafunzo.
 Mafunzo yakiendelea.
 Taswira ya chumba cha mafunzo.
 Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Maofisa Ugani ndani ya mafunzo.

Wanahabari waliopo kwenye ziara hiyo ya mafunzo wakiwa kazini.

Mtafiti, Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akiteta jambo na ofisa mwenzake, Teddy Lyimo.

WATAALAMU wa kilimo wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wametakiwa kupokea mafunzo na kuyapeleka wa wakulima ili kuwasaidia kupata mbinu mpya za uzalishaji na zinazotumia teknolojia katika kuongeza tija kwenye  uzalishaji wa mazao mbalimbali yanayolimwa kwenye maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa wilayani hapa leo na Mtafiti Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo.

Alisema ili mafunzo hayo yaweze kuleta maana kwa wakulima na Serikali hawana budi  kuyafanyia kazi kwa kwenda kuwafundisha wakulima kwa vitendo mbinu hizo za uzalishaji kwa kuanzisha mashamba madogomadogo ili wakulima waweze kuona na kasha nao kufuata kwa vitendo mbinu hizo pale watakapoona matokeo mazuri kwenye mashamba hayo ya mfano.

“COSTECH kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB) wameona waendeshe mafunzo kwa wakagani ambao ndio injini ya kilimo ili  kuwakumbusha majukumu yenu  na kuwapatia  mbinu malimbali  ili muweze kukumbuka na kutekeleza majukumu yenu vizuri maana wakulima wanawategemea nyinyi ” alisisitiza Daniel.

Alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga kuwapatia mbinu bora za uzalishaji wa mazao ya Pamba,Viazi lishe,Mihogo na nafasi ya matumizi ya bioteknolojia katika kusaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa sasa na kuongeza uzalishaji.

Kwa upande wake muwakilishi wa ofisa kilimo mkoa wa Tabora, Said Babu alisema Mkoa wao umepata bahati ya pekee kwa wataalamu wake kupata mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwaongezea ujuzi na kuwakumbusha majukumu yao.

Aliongeza Mkoa unaamini mafunzo hayo hayatapotea bure na kuishia kwenye ukumbi huo bali wanategemea kuona kilimo cha kisasa kitafanywa na wakulima na kuongeza uzalishaji kwenye msimu ujao wa kilimo kitu ambacho ndicho shabaha ya mafunzo hayo.

Alisema mazao yote matatu ya chakula ya Mahindi,Mihogo na Viazi lishe ni mazao muhimu kwa chakula kwa wakazi wa Mkoa wa Geita hivyo mafunzo hayo yawe chachu mpya katika kufanya mapinduzi kwenye kilimo na kuwataka kutumia mbinu hizo kuzalisha zao la pamba kitaalmu kuwaandaa wakulima na mpango wa serikali ya viwada.

Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo ya Uyui,  Deogratius Mwampinzi ameipongeza COSTECH na OFAB kwa kuwapelekea mafunzo hayo wataalamu wake kwani mafunzo hayo yatasaidia kuwakumbusha wataalamu hao mbinu walizojifunza vyuoni na kuwapatia mbinu zingine mpya ambazo watafiti wanaendelea kuzigundua ili kuwasaidia wakulima kila siku.

“Tutahakikisha mafunzo haya yanawafikia wakulima kwa kumfuatilia kwenye kata yake kila afisa ugani anayepata mafunzo ili kuona kama mbinu mlizowafundisha zinafahamika na kutumiwa na wakulima”Alissisitiza Mwampinzi.

Hata hivyo amewataka maofisa ugani hao kuwa wasikivu na waulize maswali katika kila mbinu wanayoona inahitaji ufafanuzi ili waweze kuondoaka hapo wakiwa wameelewa vizuri ili wakawaeleweshe wakulima kwenye maeneo yao bila wasiwasi wala kigugumizi.

Mafunzo hayo baada ya kumalizika kwenye wilaya za mkoa wa Geita sasa yanaendelea kwenye Mkoa wa Tabora na wilaya zake ambapo mpaka sasa tayari yameshafanyika kwenye wilaya za Igunga,Nzega na sasa Uyui na yataendelea kwenye wilaya za Sikonge na Urambo

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube