Bondia Conor McGregor ametamaba kummaliza katika raundi ya nne bingwa wa dunia wa ngumi za kulipwa ambaye hajawahi kupoteza pambano, Floyd Mayweather katika ufunguzi wa ziara ya promosheni ya pambano lao la Agost 26, mwaka huu mjini Los Angeles, Marekani.
Mbele ya mashabiki 11,000 ukumbi wa LA's Staples Center, Mayweather na McGregor walikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu kuthibitishwa kwa pambano lao la utajiri mkubwa.
Licha ya kutokea mbele ya umati wa mashabiki wa nyumbani na kuvaa tracksuti yenye rangi za bendera ya Marekani, lakini Mayweather alijikiuta akizomewa huku mpinzani wake kutoka Ireland, McGregor akishangiliwa kila alipotokea kwenye kioo kikubwa chaTelevisheni.
McGregor amesema kuwa ni mchezo wenye sheria zinazobana na kulifanya pambano hilo liwe nusu pambano.
Pamoja na tambo hizo bondia Mayweather naye hakuwa kimya, kwani alijibu tambo za mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anayejiandaa kwa pambano la kwanza kabisa la ngumi bila mateke kiasi cha wawili hao kukaribia kupigana 'kavu kavu'.
KWA PICHA ZAIDI GONGA HAPA>>>>>>>
No comments:
Post a Comment