Baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumuengua kocha maarufu nchini, Jamhuri Kihwelo Julio aliyekuwa anawania uongozi wa shirikisho hilo katika nafasi ya Umakamu mwenyekiti hatimaye mgombea huyo ameeleza baadhi ya mapungufu ya Kamati.
Kamati ililiondoa jina la Julio baada ya kudai kuwa hakuwasilisha baadhi ya vyeti vya elimu ya sekondari Sababu ambayo amesema haikuwa na mashiko kwani aliwahi kutoa taarifa kwa uongozi ikiwepo katika baraza la Mitiahani NECTA kuptelewa na vyeti vyake.
Aidha Julio amesema kuwa ana mashaka na Kamati hiyo kwani ilishindwa kutumia weledi kwani walipaswa kufutilia NECTA ili kutambua kuwa ni kweli ana vyeti ama laa, huku akilaumu zozezi hilo kufanywa haraka hadi yeye kuenguliwa katika nafsi aliyokuwa akigombea.
Baadaya ya kuzungumza hayo Channel ten ikataka kufahamu iwapo mgombea huyo atakata rufaa na hayo ndio majibu ya Julio.
No comments:
Post a Comment