Ibrahim Sapi Mkwawa,Msajili wa Michezo |
Akizungumza na mtandao wa Shamakala360 ofisini kwake Msajili wa Michezo Ibrahim Sapi Mkwawa, amesema kuwa madai hayo amekuwa akiyasikia kwenye vyombo vya habari, ambapo ameamua kusema taarifa sahihi juu ya yeye kupitisha katiba ya marekebisho kwani alichofanya ni kuhariri na kupunguza baadhi ya vifungu vya katiba ambavyo vilikuwa vinajirudia rudi.
Amesema kuwa hakuna katiba mpya iliyopelekwa kwake bali alifikishiwa katiba ya Simba kuihariri ambapo pale alipona kuna mapungufu aliirejesha kwa viongozi wa Simba ili kupunguza mapungufu aliyoyaona.
Aidha ameenda mbali kwa kusema baadhi ya mambo ambayo yalikosewa ndio yaliyomfanya kuwarejeshea viongozi wa Simba Katiba ili ifanyiwe uhariri tena, ambapo pia amesema malalamiko hayo.
No comments:
Post a Comment