BREAKING

Tuesday 11 July 2017

KOCHA MAYANGA AYAWEKA HADHARANI MAJINA 24 YA WACHEZAJI WATAKAOWAKABILI RWANDA-MWANZA


Kocha Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wacheaji 24 kitakacho menyana na na Rwanda Jijini Mwanza katika mchezo wa CHAN huku akiwaacha abaadhi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho.

Mayanga amemuondoa kipa wa Yanga, Benno Kakolanya katika kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na kumchukua chipukizi, ambaye alikuwa katika kikosi Serengeti Boys Ramadhani Kabwili kwa ajili ya mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda Jumamosi.

Taifa Stars wataanza kampeni za kuwania kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee kwa mara ya pili baada ya mwaka 2009 nchini Ivory Coast kwa kumenyana na Amavubi Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Akizungumzia mabadiliko hayo kocha Mayanga amesema amemuondoa Kakolanya na kumchukua kipa wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyoshiriki Fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu, Kabwili aliyeonyesha uwezo mkubwa kwenye michuano hiyo.

Katika hatua nyingine Kaocha mayanga amempongeza kipa Said Mohamed kwa kutwaa tuzo ya kipa bora kwani ameiletea sifa kubwa nchini na heshima kwa SWtars baada ya kufanya vyema katika mchezo wake dhidi ya Lesotho.

Kikosi hicho kimeondoka Dar es Salaam,  kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube