BREAKING

Monday, 17 July 2017

AFISA HABARI WA KLABU YA SOKA YA SIMBA HAJJI MANARA ATANGAZWA NA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF KUWA HURU KATIKA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA ALICHOPEWA.

ABBASI TARIMBA Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu(TFF).
Hatimaye Afisa habari wa klabu ya soka ya simba Hajji Manara sasa yupo huru baada ya Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania(TFF) Abbasi Tarimba,kutangaza kusamehewa makosa aliyotenda na kupelekea kufungiwa.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti huyo wa kamati hiyo amesema kuwa kamati imetoa msamaha wa adhabu iliyokuwa ikiwakabili watuhumiwa wanne ndani ya shirikisho hilo akiwepo Manara pamoja na James Makwimla, Ayubu Nyaulingo na Glas Kiondo waliyoadhibiwa kutokana na tuhuma mbalimbali za utovu wa nidhamu, ikiwepo kuingilia kazi za viongozi wa TFF

Tarimba amesema kamati imeridhia kutoa msamaha huo kufutia wadhibiwa hao kuomba msama kwa yaliyotokea ambapo sasa kila mmoja yupo huru na wanaweza kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa awali.

Aidha Tarimba akaongeza kuwa msamaha huo uliotolewa na kamati hautomhusu mtu yeyote ambaye aliadhibiwa ambaye hajaomba, ama aliyekata rufaa lakini bado akawa amekataliwa ama kwa hali yoyote, isipokuwa kwa wale wote walioomba msamaha ambao sasa wapo huru

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube