MSAMA-Mkurugenzi wa Msama Auction Mart. |
Kampuni hiyo kepitia Mkurugenzi wake Alex Msama imesema inaungana na Serikali kuhakikisha wezi wa kazi za wasanii sasa inakuwa vita kwani wasanii wengi wamekuwa wakidhulumiwa kwa kiasi kikubwa.
Akizungumzia sula hilo Mkurugezi wa Msama Promosheni amesema kuwa watakaohusika katika zoezi hilo la kuwakamata ni pamoja na wale wanadurufu CD feki, pamoja na wale wanaonyonya nyimbo kwa kutumia kompyuta .
Amesema kuna vijana wengi wanafanya kazi hiyo na kurudisha nyuma maendeleo ya wasanii, ambao wamekuwa wakilia kila kukicha juu ya wizi huo.
No comments:
Post a Comment