BREAKING

Saturday, 29 July 2017

MASHINDANO YA KIGWANGALLA CUP 2017 YAZINDULIWA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI

 
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na timu ya Kata ya Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wachezaji wa Kata ya Nkiniziwa wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wachezaji wa timu za Kata za Nkiniziwa na Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.

Mtanange baina ya Mzimaziba dhidi ya Nkiniziwa ukiendelea katika mchezo wa ufunguzi wa Kigwangalla Cup 2017

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu za Nkiniziwa na Mzibaziba (Msibasiba) wakati wa ufunguzi huo.

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wananchi waliojitokeza kwenye tukio hilo la ufunguzi wa Kigwangalla Cup 2017

Wazee wakicheza mchezo wa bao la asili la kabila la Wanyamwezi wakati wa sherehe za uzinduzi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017

Timu zikichuana mchezo wa drafti

Wazee wakishindana katika kuwania kukimbiza Kuku

Hatmaye kuku alinyakuliwa na mshindi

Mashindano ya kukumbia mita 100

Timu ya Wazee Nzega Vijijini wakipata picha ya pamoja

timu ya Madiwani wa Jimbo la Nzega Vijijini wakiwa kwenye picha ya pamoja

Mtanange huo ukiendelea kati ya timu ya Madiwani wa Jimbo la Nzega Vijijini na Wazee wa Nzega Vijijini

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwapongeza Madiwani wa Jimbo laNzega Vijijini mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kirafiki ambapo timu ya Madiwani waliibuka kwa ushindi mnono wa bao 1-0.

Wachezaji wa timu ya Mzibaziba (kushoto) pamoja na timu ya Nkiniziwa (kulia) wakiingia uwanjani wakati wa mchezo huo maalum wa ufunguzi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017.

Mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za Kata zilizo ndani ya Jimbo la Nzega Vijijini maalufu kama ‘Kigwangalla Cup’ yamezinduliwa rasmi jioni ya Julai 27, 2017 huku miamba 20 ikitarajiwa kuumana kumpata bingwa wa Jimbo hilo kwa mwaka huu. Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliwataka wachezaji wote wanaoshiriki michuano hiyo kuwa na nidhamu iliwaitumie michuano hiyo kama kipimo cha wao cha kuonesha vipaji vyao ili waonekane ngazi za juu. “Mpambane kweli kweli. Kila mmoja wenu aoneshe uwezo wake wa kusakata kabumbu. Pia muzingatie nidhamu ya hali ya juu kwani michezo inaleta umoja na amani, inaimalisha afya ya miili yetu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati akuzungumza na wachezaji katika ufunguzi wa michuano hiyo. Dk. Kigwangalla pia alipata wasaha wa kukagua timu zilizofungua rasmi michuano hiyo kati ya Mizibaziba dhidi ya Nkiniziwa ambazo hata hivyo mpaka kipyenga cha mwisho zilitoka droo ya bao 1-1. Dk. Kigwangalla alieleza kuwa, jumla ya Kata 19 za jimbo lake hilo zimeweza kutoa timu ilikushiriki michuano hiyo huku timu maalum ikiingizwa ambayo itajumuisha Madiwani wote kutoka Kata hizo ili kufanya jumla ya timu 20. Dk. Kigwangalla alizitaja baadhi ya Kata zinazochuana kwenye michuano hiyo ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata, Sanzu,Lusu, Milambo Itobo, Magengati,Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi. Kata zingine ni Kata za Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala. Awali kabla ya kuanza rasmi kwa mchezo wa ufunguzi, Madiwani wa Kata zote waliweza kukabidhiwa baadhi ya vifaa kwa timu zao sambamba na hilo wananchi waliweza kufurahia michezo mbalimbali ikiwemo ile ya jadi hasa mchezo wa asili wa bao la Kinyamwezi, kucheza drafti, kukimbiza kuku, michezo ya mbio kwa Wazee huku mchezo wa mbio kwa watu wenye vitambi ukitia fola kwenye ufunguzi huo, uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Nkiniziwa iliyopo kwenye Kata hiyo ya Nkiniziwa.


Monday, 24 July 2017

TAMASHA KUBWA LA CASTLE LITE UNLOCKS LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM



Msanii Vanessa Mdee akiwa jukwaani akiwakonga mashabiki.

MAOFISA UGANI WATAKIWA KUTUMIA MAFUNZO WANAYOPATA KUWAELIMISHA WAKULIMA


Mtafiti, Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akizungumza na maofisa ugani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa maofisa hao kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo Mkoani Tabora leo.

Monday, 17 July 2017

CHAMA CHA RIADHA TANZANIA RT CHATANGAZA KUHAIRISHA MASHINDANO YA TAIFA KUFUTIA UKATA WA FEDHA.

WILHELM  GIDABUDAY-Katibu Mkuu wa RT


Katibu Mkuu wa Chama caha Riadha tanzania RT Wilhelm GidaBuday amesema kuwa kufuatia ukata wafedha wanaokabiliana nao wameamua kustisha mashaindano ya Taifa ambayo yalitakiwa kuanza kutimua vumbi Kibaha Mkani Pwani Julai 22 mwaka hu.

Gidabuday amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari akisema kufutia mwingiliano wa mashindano makubwa duniani yakiwepo mashindano ya dunia yanayofanyika hivi karibuni Uingereza pamoja na yale Bahamas, ambapo tayari wanariadha wamesafiri kuiwakilisha Tanzania, pamoja na yale ya Jamaica

Ameema kufuatia mwingiliano huo wameona ni vyema kuhairisha mashindano hayo ya Taifa hadi hapo yatakapotangazwa kwa mara nyingingi, huku akiwasihi wanariadha kuendelea kujifua zaidi.

Tayari baadhi ya wachezaji channel ten imewashuhudia wakijifua katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mshindano ya Taifa ambayo yalikuwa yaanze Julai 22, lakini kuhairishwa kwa mashindano hayo sasa wanariadha hao watarejea katika vituo vyao.

VITA YA WEZI WA KAZI ZA WASANII,MSAMA AJITOSA TENA


MSAMA-Mkurugenzi wa Msama Auction Mart.
Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart, inatarajia kuanza kuwakamata wezi wote wanaojishughulisha na wizi wa kazi za wasanii, ambapo itaanza kazi hiyo Jumatatu ya wiki inayokuja.

Kampuni hiyo kepitia Mkurugenzi wake Alex Msama imesema inaungana na Serikali kuhakikisha wezi  wa kazi za wasanii sasa inakuwa vita kwani wasanii wengi wamekuwa wakidhulumiwa kwa kiasi kikubwa.

Akizungumzia sula hilo Mkurugezi wa Msama Promosheni amesema kuwa watakaohusika katika zoezi hilo la kuwakamata ni pamoja na wale wanadurufu CD feki, pamoja na wale wanaonyonya nyimbo kwa kutumia kompyuta .

Amesema kuna vijana wengi wanafanya kazi hiyo na kurudisha nyuma maendeleo ya wasanii, ambao wamekuwa wakilia kila kukicha juu ya wizi huo.

AFISA HABARI WA KLABU YA SOKA YA SIMBA HAJJI MANARA ATANGAZWA NA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF KUWA HURU KATIKA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA ALICHOPEWA.

ABBASI TARIMBA Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu(TFF).
Hatimaye Afisa habari wa klabu ya soka ya simba Hajji Manara sasa yupo huru baada ya Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania(TFF) Abbasi Tarimba,kutangaza kusamehewa makosa aliyotenda na kupelekea kufungiwa.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti huyo wa kamati hiyo amesema kuwa kamati imetoa msamaha wa adhabu iliyokuwa ikiwakabili watuhumiwa wanne ndani ya shirikisho hilo akiwepo Manara pamoja na James Makwimla, Ayubu Nyaulingo na Glas Kiondo waliyoadhibiwa kutokana na tuhuma mbalimbali za utovu wa nidhamu, ikiwepo kuingilia kazi za viongozi wa TFF

Tarimba amesema kamati imeridhia kutoa msamaha huo kufutia wadhibiwa hao kuomba msama kwa yaliyotokea ambapo sasa kila mmoja yupo huru na wanaweza kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa awali.

Aidha Tarimba akaongeza kuwa msamaha huo uliotolewa na kamati hautomhusu mtu yeyote ambaye aliadhibiwa ambaye hajaomba, ama aliyekata rufaa lakini bado akawa amekataliwa ama kwa hali yoyote, isipokuwa kwa wale wote walioomba msamaha ambao sasa wapo huru

MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO AWAKANA WAZEE WA KLABU YA SOKA YA SIMBA JUU YA KATIBA..

Ibrahim Sapi Mkwawa,Msajili wa Michezo 
Siku Chache tangu wazee wa klabvu ya soka ya Simba kuibuka kwa kumuomba Rais John Pombe Magufuli kuingilia katika maamuzi mabovu ndani ya klabu ya soka ya simba ikiwepo kufanya marekebisho ya katiba bila mkutano mkuu pamoja na kutosomewa baadhi ya mapato na matumizi hatimaye msajili wa Vyama vya Michezo ameibuka na kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo.

Akizungumza na mtandao wa Shamakala360 ofisini  kwake Msajili wa Michezo Ibrahim Sapi Mkwawa, amesema kuwa madai hayo amekuwa akiyasikia kwenye vyombo vya habari, ambapo ameamua kusema taarifa sahihi juu ya yeye kupitisha katiba ya marekebisho kwani alichofanya ni kuhariri na kupunguza baadhi ya vifungu vya katiba ambavyo vilikuwa vinajirudia rudi.

Amesema kuwa hakuna katiba mpya iliyopelekwa kwake bali alifikishiwa katiba ya Simba kuihariri ambapo pale alipona kuna mapungufu aliirejesha kwa viongozi wa Simba ili kupunguza mapungufu aliyoyaona.

Aidha ameenda mbali kwa kusema baadhi ya mambo ambayo yalikosewa ndio yaliyomfanya kuwarejeshea viongozi wa Simba Katiba ili ifanyiwe uhariri tena, ambapo pia amesema malalamiko hayo.

UMIA NI CHACHU KWA UKUAJI WA BIASHARA ZA MTANDAONI BARANI AFRIKA



Mwaka 2017 kampuni ya Jumia ambayo inajishughulisha na huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao barani Afrika inatimiza miaka mitano tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2012.

Kampuni hiyo ambapo awali ilikuwa ikijulikana kama Africa Internet Group (AIG) pindi inaanzishwa imejikita zaidi na shughuli zake mtandaoni katika maeneo kama ya huduma za chakula (Jumia Food), manunuzi ya bidhaa mbalimbali (Jumia Market), hoteli na usafiri wa ndege (Jumia Travel), makazi (Jumia House), magari (Jumia Cars), matangazo (Jumia Deals) na kazi (Jumia Jobs).
Katika kuzikabili changamoto zinazolikabili bara la Afrika kama vile miundombinu hafifu kama vile usafiri wa barabara na anga, umbali wa maeneo na foleni ndefu za barabarani ambazo husababisha watu kupoteza muda mwingi kufika maeneo mbalimbali zote hizi zinatoa fursa kwa kutumika njia ya mtandao wa intaneti ili kuokoa muda na gharama.

Wednesday, 12 July 2017

MICHAEL CARRICK AMRITHI KITAMBAA WAYNE ROONEY

Manchester United imemtangaza nyota we  Michael Carrick kuwa nahodha mpya akichukua mikoba ya aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho Wayne Rooney ambaye amejiunga na Everton, na nafasi hiyo kukabidhiwa kiungo huyo mzoefu.

Carrick pamoja na kikosi kizima cha Manchester kwa sasa kipo katika maandalizi ya Ligi Kuu ya Uingereza ambayo itaanza mwezi ujao, na katika mazoezi ya jana nyota huyo alionekana mwenye furaha kila wakati.






KWA PICHA ZAIDI GONGA HAPA>>>>

CONOR MCGREGOR ATAMBA KUMTWANGA BINGWA WA DUNIA FLOYD MAYWEATHER


 Bondia Conor McGregor ametamaba kummaliza katika raundi ya nne bingwa wa dunia wa ngumi za kulipwa ambaye hajawahi kupoteza pambano, Floyd Mayweather katika ufunguzi wa ziara ya promosheni ya pambano lao la Agost 26, mwaka huu mjini Los Angeles, Marekani.

Mbele ya mashabiki 11,000 ukumbi wa LA's Staples Center, Mayweather na McGregor walikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu kuthibitishwa kwa pambano lao la utajiri mkubwa.

Licha ya kutokea mbele ya umati wa mashabiki wa nyumbani na kuvaa tracksuti yenye rangi za bendera ya Marekani, lakini Mayweather alijikiuta akizomewa huku mpinzani wake kutoka Ireland, McGregor akishangiliwa kila alipotokea kwenye kioo kikubwa chaTelevisheni. 

McGregor amesema kuwa  ni mchezo wenye sheria zinazobana na kulifanya pambano hilo liwe nusu pambano. 

Pamoja na tambo hizo bondia  Mayweather naye hakuwa kimya, kwani alijibu tambo za mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anayejiandaa kwa pambano la kwanza kabisa la ngumi bila mateke kiasi cha wawili hao kukaribia kupigana 'kavu kavu'.
KWA PICHA ZAIDI GONGA HAPA>>>>>>>

Tuesday, 11 July 2017

JULIO AICHAMBUA KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF, ASEMA IMEKURUPUKA KUMKATA......


Baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumuengua kocha maarufu nchini, Jamhuri Kihwelo Julio aliyekuwa anawania uongozi wa shirikisho hilo katika nafasi ya Umakamu mwenyekiti hatimaye mgombea huyo ameeleza baadhi ya mapungufu ya Kamati.

Kamati ililiondoa jina la Julio baada ya kudai kuwa hakuwasilisha baadhi ya  vyeti vya elimu ya sekondari Sababu ambayo amesema haikuwa na mashiko kwani aliwahi kutoa taarifa kwa uongozi ikiwepo katika baraza la Mitiahani NECTA kuptelewa na vyeti vyake.

Aidha Julio amesema kuwa ana mashaka na Kamati hiyo kwani ilishindwa kutumia weledi kwani walipaswa kufutilia NECTA ili kutambua kuwa ni kweli ana vyeti ama laa, huku akilaumu zozezi hilo kufanywa haraka hadi yeye kuenguliwa katika nafsi aliyokuwa akigombea.

Baadaya ya kuzungumza hayo Channel ten ikataka kufahamu iwapo mgombea huyo atakata rufaa na hayo ndio majibu ya Julio.

KOCHA MAYANGA AYAWEKA HADHARANI MAJINA 24 YA WACHEZAJI WATAKAOWAKABILI RWANDA-MWANZA


Kocha Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wacheaji 24 kitakacho menyana na na Rwanda Jijini Mwanza katika mchezo wa CHAN huku akiwaacha abaadhi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho.

Mayanga amemuondoa kipa wa Yanga, Benno Kakolanya katika kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na kumchukua chipukizi, ambaye alikuwa katika kikosi Serengeti Boys Ramadhani Kabwili kwa ajili ya mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda Jumamosi.

Taifa Stars wataanza kampeni za kuwania kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee kwa mara ya pili baada ya mwaka 2009 nchini Ivory Coast kwa kumenyana na Amavubi Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Akizungumzia mabadiliko hayo kocha Mayanga amesema amemuondoa Kakolanya na kumchukua kipa wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyoshiriki Fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu, Kabwili aliyeonyesha uwezo mkubwa kwenye michuano hiyo.

Katika hatua nyingine Kaocha mayanga amempongeza kipa Said Mohamed kwa kutwaa tuzo ya kipa bora kwani ameiletea sifa kubwa nchini na heshima kwa SWtars baada ya kufanya vyema katika mchezo wake dhidi ya Lesotho.

Kikosi hicho kimeondoka Dar es Salaam,  kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

WAZIRI MWAKYEMBE ASITISHA UTEUZI WA MALINZI WA BMT NA WAJUMBE WOTE BMT



DK.HARRISON MWAKYEMBE-Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akizunggumza na wanahabari hawapo pichani, kutangaza kuengua safu ya Uongozi wa BMT

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, DK. Harrison Mwakyembe amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi pamoja na wajumbe wote wa baraza hilo.

Waziri Mwakyembe amechukua uamuzi huo leo Jumatatu katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kufuatia agizo la waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati wa hotuba yake ya kufunga bunge, kuvunjwa kwa BMT kama haitaonekana kuwa na utendaji mzuri.

Licha ya kusitisha uteuzi wa mwenyekiti wa baraza hilo waziri huyo pia amesitisha uteuzi wa wajumbe wote katika baraza hilo huku sekretarieti ikipewa jukumu la kuendelea na kazi zake kwa kushirikiana na serikali wakati ikijipanga kwa ajili kuanza mchakato wa kutafuta viongozi wapya.

Wakati Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wake Dk John Pombe Magufuli, wakati ikiingia madarakani ilieleza nia yake thabiti ya kuendeleza michezo na kufanya sehemu ya ajira kwa vijana hususani wenye vipaji vya michezo pamoja na kupunguza migogoro ambayo ilikuwa ikijitokeza mara kwa mara..

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JUNI,2017 WAPUNGUA KWA ASIMILIA 5.4


 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigwabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leokuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Juni. Kulia  ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira, Ruth Minja.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni  umepungua hadi kufikia asilimia 5.4 ikilinganishwa na asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Mei 2017.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko huo wa bei.

Kwasigabo alisema kasi hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2017 imepungua zaidi ikilinganishwa na kasi iliyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2017.

"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.10 mwezi Juni,2017 kutoka 103.47 mwezi Juni 2016" alisema Kwesigabo.

Alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Juni 2017 umepungua hadi hadi asilimia 9.6 kutoka asilimia 11.6 ilivyokuwa mwezi Mei,2017

Alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Juni 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 9.8 kutoka asilimia 11.8 mwezi Mei 2017.

Aliongeza kuwa badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa zisizo za vyakula umeongezeka hadi asilimia 3.11 mwezi Juni 2017 kutoka asilimia 3.1 mwezi Juni, 2017 kutoka asilimia 3.0 mwezi Mei 2017.

Wednesday, 5 July 2017

YANGA YAMTAMBULISHA NYOTA WAO IBRAHIM AJIBU, PASTORY ATHANAS AJIUNGA NA SINGIDA UNITED

Ajibu akikabidhiwa Jezi yake namba 10 kwa ajili ya kutumikia Yanga msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara

Mshambuliaji Pastory Athanas

MANISPAA YA UBUNGO YAANZISHA REJESTA YA WAKAZI KWA KILA MTAA


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akionyesha kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali muda mchache mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba CCM. Leo June 5, 2017

 Mfano wa Fomu ya huduma kwa mwananchi (Fomu ya malalamiko)

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kuelezea dhima ya kuanzisha Daftari la wakazi wa kila Mtaa katika Manispaa ya Ubungo.Leo June 5, 2017

 Kitabu cha Kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika ofisi za serikali


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kuelezea dhima ya kuanzisha Daftari la wakazi wa kila Mtaa katika Manispaa ya Ubungo.Leo June 5, 2017


 Mfano wa Fomu ya Rejista ya Wakazi katika kila Mtaa


Ili kupunguza uhalifu katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam imebainika kuwa ni vyema kuwatambua wananchi wote na mahali wanapoishi ikiwemo kubaini wageni wote wanaowasili katika Manispaa ya Ubungo ikiwa ni pamoja na mahali wanapofikia.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kibamba Chama Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa  kumekuwa na uhalifu kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali Katika Manispaa hiyo jambo ambalo limetafutiwa muarobaini kwa kuanzishwa daftari la wakazi litakalobainisha wakazi wote ili kukitokea uhalifu iwe rahisi kuwabaini wahalifu hao.
Kuanzishwa kwa Daftari la Rejesta ya Wakazi wa Mtaa ni agizo lililotolewa hivi karibuni na MKUU wa Wilaya ya Temeke Mhe Felix Lyaviva kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa za Kigamboni, Ilala, Temeke, Kinondoni na Ubungo wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda katika ufunguzi wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ili kuwaelimisha watumiaji wa Intaneti wapatao milioni 20 sambamba na watumiaji wa simu za mikononi wapatao milioni 40 kuwa na matumizi bora ya simu za mikononi na mitandao ya kijamii.
Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amesema kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Daftari la Rejesta ya wakazi wa Mtaa pia kutakuwa na Fomu ya Rufaa ya Malalamiko katika kila Mtaa sambamba na kitabu cha kutunza kumbukumbu za kusikiliza malalamiko ya wananchi katika Ofisi za serikali.

Tayari vitabu hivyo vyote vimeanza kugawanywa katika kila Mtaa ili kuanza utekelezaji wa zoezi hilo haraka iwezekanavyo.


IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO 
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube