BREAKING

Wednesday 23 August 2023

PROF: HAMISI M. MALEBO AZUNGUMZIA UHAMISHAJI WANANCHI KATIKA HIFADHI YA NGORONGORO


’Uthibiti wa Magonjwa ya binadamu katika eneo la hifadhi ni changamoto kubwa, mbinu ambazo tunaweza kuzitumia nje ya hifadhi hatuwezi kuzitumia ndani ya hifadhi, kulingana na sheria za uhifadhi, katika eneo la ndani ya hifadhi hatuwezi kupulizia dawa ni mambo yasiyoruhusiwa, sasa Mwananchi anapokuwa pale analiletea pia Taifa changamoto kubwa ya namna ya kuendelea kumuhudia wakati yupo kwenye eneo ambalo lina vikwazo vingi katika masuala ya huduma za Afya na za Kijamii.

Wengine watashangaa kwamba kwa nini haya magonjwa tunayataja sana kwa Ngorogoro, maeneo mengine pia yapo lakini Ngorongoro ni eneo ambalo hawa wananchi wapo katika maeneo ambayo yamejitenga kuwafikia katika maeneo yao ni changamoto sana, kwa hiyo ule ugumu wa kuwapa huduma unawafanya waendelee kuteseka na magonjwa ambayo yanathibitika ni magonjwa ambayo tunaweza kuyakinga na kuyaondoa, tunaona Wananchi wanaishi katika hifadhi ya Ngorongoro lakini ukienda Mataifa mengine huwezi kukuta Wanadamu wanaishi katikati ya Wanyama pori.

Magonjwa yapo sehemu nyingine lakini kiwango cha Magonjwa katika hifadhi ya Ngorongoro ni kikubwa, ukiangalia changamoto anazozipata Mtoto mdogo wa chini ya miaka mitano aliyeko Ngorongoro ni kubwa kuliko Mtoto aliyeko Dar- es Salaam, Mwanza, Morogoro na sehemu nyingine, kwa mtu yeyote anayedhamini na kuheshimu ubinadamu kama angeweza kutembelea yale maboma na kuona maisha wanayoishi hawa watoto wadogo, hawana hata uhuru wa kucheza kwa sababu akisogea mita 5 tu anaweza kupitiwa na fisi, chui, Simba na wanyama wengine wakali yani hawa ni Watanzania wenzetu ambao wapo kwenye mazingira magumu na ya kutisha kwa mtu yeyote mwenye moyo wa huruma atafikiria tofauti’’.

Profesa Hamis ameseyasema hayo wakati alipokuwa katika  Mkutano wa mtandao wa Zoom, akizungumzia kuhusu awamu ya pili ya uhamishaji wananchi katika Hifadhi ya Ngorongoro

**HABARI HII KWA HISANI YA GILLY BONNY*****


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube