MAKALA MAALUM-ZIARA YA KINANA
NA SAID MAKALA
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Abdulrhamani Kinana hivi karibuni aliihitimisha ziara yake ya ya siku 10 katika mikoa mitano,ziara ambayo ilikuwa mahususi katika utelezaji wa Ilani ya Chama hicho tawala cha CCM.
Katika Mikoa hiyo Kanali huyo mstaafu alizungumza mambo mengi kwa wanachi waiofurika katika mikutano yake ya hadhara lakini mengi yakiwa yamejaa utamu wa chakula cha akili kama mfano wa muwa uliojaa maji mengi na mtamu mithili ya asali , huku ukitafsirika kuwa na vikonyo kede kede shinani.
Katika ziara hiyo niliambatana naye niliona mengi ya kujifunza kutoka kwa Mwansiasa huyu nguli ambaye ama hakika ni wa kupigiwa mfano , katika ziara zake hizi si mara ya kwanza kuhuhudhuria huwa naburudika na maneno yake ya hekima yaliyojaa matumaini na hamasa ya kufufua fikra ambazo zilianza kufa kw awananchi ambao pengine katika maendeleo yao ya kiuchumi wanakutana na changamoto kadha wa kadha.
Akiwa Butiama Mkoani Mara nilimshuhudia kwa mara nyingine mzee Kinana akitoa tafsiri kubwa ya kuwaenzi mashujaa ambao wameipambania Tanzania katika kuleta ukombozi kutoka kwa Taifa jirani la Uganda, nakumbuka maneno haya aliyasema hivi
"Tuendelee kuwaenzi mashujaa walioshiriki katika vita vya ukombozi dhidi ya nduli Idd Amin na shujaa wa kwanza ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye atabaki kuwa kielelezo wa Taifa la Tanzania"
Maneno hayo yalinikumbusha maneno ya hekima na Buasara wakati Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini ambaye alichaguliwa kidemokrasia na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, ambaye alifariki Desemba 5, 2013 akiwa na umri wa miaka 95.
Mandela anatambuliwa na taifa la Afika Kusini kwa kuleta mapinduzi ya Kiasisa kwani aliwahi kufungwa kwa kutumikia kifungo kwa miaka 27 kwa sababu ya mapambano yake dhidi ya mfumo wa kibaguzi wa Afrika Kusini unaofahamika kama Ukaburu. Aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 1990, na kuwa rais miaka minne baadae, na kuachia madaraka baada ya kutumikia kwa kipindi kimoja tu, kitendo adimu kufanywa na wenye madaraka barani Afrika.
Akiwa mtu anayependwa duniani kote, Mandela alikuwa na namna ya mvuto katika maneno yake, Moja ya nukuu zake inatoka katika hotuba yake ya kijeuri aliyoitoa mahakamani wakati wa kesi maarufu ya Uhaini ya Rivonia mwaka 1964, ambapo. alisema "Nimepigana dhidi ya mfumo wa utawala unaowapendelea makaburu, na nimepigana dhidi ya mfumo wa utawala unaowapendela weusi. Nimekuwa na ndoto ya jamii ya kidemokrasia na huru ambayo watu wote wanaishi pamoja kwa mshikamano na fursa sawa. Ni ndoto ambayo nataraji kuiishi na kuitimiza. Lakini, kama itahitajika, hiyo ni ndoto ambayo nimejiandaa kupoteza maisha yangu kwa ajili yake."
Ukiacha hotuba hiyo ya kesi yake ya Rivonia, Mandela anaacha nyuma yake nukuu nyingi za kukumbukwa zenye busara alizozitoa katika kipindi chake chote cha uhai wake. Pamoja na kutuacha, anaendelea kuzungumza na ulimwengu kupitia watumiaji wa twita, ambao waliitikia habari za kifo chake kwa kusambaza maneno yake.
Maneno hayo ni ninayakumbuka sana kwa kuwa Mzee Kinana anendelea kutukumbusha na yeye ni mmoja wa watu wenye msimamo wa kusimamia maneno yenye Busara mtu ambaye hapendi kukwezwa, hata wasaidizi wake wanatambua hilo lakini mtu ambaye anatamani kuona mtanzania anapata haki ya kujenga historia bora ya kiuchumi.
No comments:
Post a Comment