BREAKING
ROSE MHANDO :MSAMA NI BABA KWANGU ACHENI KUNIGOMBISHA NAYE.   UPANDIKIZAJI WA MENO BANDIA KWA NJIA YA KISASA MUHIMBILI MLOGANZILA 45 KUNUFAIKA NA HUDUMA    UTEKAJI WA WATOTO MKUU WA MKOA WA MBEYA JUMA HOMERA AWATAKA WANAFUNZI WA HOLY LAND PRE- & PRIMARY SCHOOL KUKATAA LIFTI   MSAMA ANG'AKA WAIMBAJI WA IN JILI KUPOTOKA MAADILI   DCEA YAFANIKIWA OPERESHENI DAWA ZA KULEVYA YAKAMATA JAHAZI DAWA ZA KULEVYA   NAIBU WAZIRI MKUU AKARIPIA UZEMBE TANESCO   MHE. RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZA NA RAIS WA CHINA MHE. XI JINPING    MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI CHINA..   RAIS SAMIA NCHINI KENYA-ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI   RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA-KENYA    Blogger Tips and Tricks & Blogger Templates

Wednesday, April 09, 2025

Wednesday, 2 August 2023

KINANA: WAPINZANI JENGENI HOJA, ACHENI KEJELI KWA RAIS’.






MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinanaa amewashauri na kuwakumbusha wanaiasa wa upinzani kuheshimu fursa ya maridhiano ya kisiasa iliyotolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Amesema lugha za matusi, kejeli na dharau dhidi kiongozi wa nchi zinapaswa kuepukwa ili kutoa fursa ya kuendeleza maridhiano na kuijenga Tanzania kwa pamoja.


Kinana ameyasema hayo jana mjini Tabora wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Mara, Simiyu na Tabora kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 na uhai wa Chama.


"Niwasihi ndugu hatukatai mtoe hoja, hatukatai mseme yale mnayotaka kusema lakini semeni kwa uungwana, zungumzeni kwa busara, jengeni hoja.


"Kusema Rais ana akili za matope au kusema Rais ameuza bandari, wewe sema mkataba huu haujakaa  vizuri, utaeleweka, toa hoja kwa nini hauajakaa vizuri, upande wa pili watasema umekaa vizuri, lakini ukisema mkataba huu hata kichaa hawezi kuubali, maana nyingine unatuambia sisi sote ni vichaaa."


Kinana alitumia fursa hiyo kuelezea mchakato wa kupata maridhiano ambayo yametoa fursa ya wananchi wakiwamo wanasiasa kuwa na uhuru wa kutoa maoni.


"Kabla ya hapo mtakumbuka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alikuwa jela, Rais (Dk . Samia) kabla ya kesi haijamalizika akaamua kumwalika Ikulu...wakazungumza, wakakubaliana kwamba tujenge amani na umoja, hatimaye mazungumzo ya Chamwino yakazaliwa. Rais akaunda timu ya watu 10, watano CCM na watano Chadema. Leo nayasema haya  kwa sababu mimi ni Mwenyekiti kwa upande wa CCM katika mazungumzo hayo ya maridhiano. Mwenyekiti mwenzangu Freeman Mbowe yeye aliongoza upande wa pili na walikuja na hoja 15," amesema. 

 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube