Muonekano wa Bwawa la Julius Nyerere |
Mkurugenzi wa Tanesco Maharage Chande akizungumza katika mradi wa Bwawa la kufua Umeme wa Julius Nyerere
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limesema tayari hatua ya kwanza ya wafanyakazi 20 kati ya wafanyakazi zaidi ya 200 wanaotarajiwa kuwasili katika mradi wa uzalishaji Umeme waJulius Nyerere wamefika katika mradi huo.
Mkurugenzi wa TANESCO ,amesema hayo baada ya kuongoza jopo la menejimenti ya shirika hilo kujionea maendeleo ya mradi huo wa uzalishaji Umeme,ambapo amesema kwamba wafanyakazi hao ni wa kada mbalimbali ambao watakuwa wakifanya majukumu yao ndani ya mradi huo.
Akizungumzia taarifa ya Mamlaka ya hali ya hewa TMA juu ya uwepo wa mvua kubwa za Vuli ,amesema kuwa kama zitakuwepo uwezekano wa bwawa hilo kujaa ni mkubwa ,huku akisema iwapo hazitakuwa na athari.
Katika hatua nyingine Chande akazungumzia maendeleo ya mradi kwa ujumla na kasi yake ,kama anavyobainisha huku baadhi ya watumishi wa Shirika hilo nao wakizungumzia maendeleo ya mradi huo
No comments:
Post a Comment