BREAKING

Friday 25 August 2023

TANESCO YAONGEZA WATAALAM 20 MRADI WA BWAWA LA JNHPP



Muonekano wa Bwawa la Julius Nyerere






Mkurugenzi wa Tanesco Maharage Chande akizungumza katika mradi wa Bwawa la kufua Umeme wa Julius Nyerere









 Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limesema tayari hatua ya kwanza ya wafanyakazi 20 kati ya wafanyakazi zaidi ya 200 wanaotarajiwa kuwasili katika mradi wa  uzalishaji Umeme waJulius Nyerere wamefika katika mradi huo.

Mkurugenzi wa TANESCO ,amesema hayo baada ya kuongoza jopo la menejimenti ya shirika hilo kujionea maendeleo ya mradi huo wa uzalishaji Umeme,ambapo amesema kwamba wafanyakazi hao ni wa kada mbalimbali ambao watakuwa wakifanya majukumu yao ndani ya mradi huo.

Akizungumzia taarifa ya Mamlaka ya hali ya hewa TMA juu ya uwepo wa mvua kubwa za Vuli ,amesema kuwa kama zitakuwepo  uwezekano wa bwawa hilo kujaa ni mkubwa ,huku akisema iwapo hazitakuwa na athari.

Katika hatua nyingine Chande akazungumzia maendeleo ya mradi kwa ujumla na kasi yake ,kama anavyobainisha huku baadhi ya watumishi wa Shirika hilo nao wakizungumzia maendeleo ya mradi huo

Wednesday 23 August 2023

KINANA: UHURU WA KUSEMA UPO ILA KILA UHURU UNA MIPAKA YAKE.







MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema ingawa inchi ina uhuru mkubwa wa kusema na kutoa maoni, lakini ni vyema ukazingatia mipaka.

Kinana ameyasema hayo leo Agosti 22, 2-23 jijini Dar es Salaam wakati katika mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). 

“Mimi nadhani uhuru wa kusema upo lakini kila uhuru una mipaka yake, Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere) alikuwa akitufundisha kwamba uhuru bila ya nidhamu ni wendawazimu na nidhamu bila ya uhuru ni utumwa, kwa hiyo kila uhuru lazima uwe na mipaka yake lakini nadhani kwa ujumla uhuru upo wa kutosha wakati mwingine labda kuna kasoro katika utekelezaji wake nadhani ndio maana Watanzania wanapiga kelele katika kusimamia sheria zinazowapa Watanzania uhuru wa kusema.



 

PROF: HAMISI M. MALEBO AZUNGUMZIA UHAMISHAJI WANANCHI KATIKA HIFADHI YA NGORONGORO


’Uthibiti wa Magonjwa ya binadamu katika eneo la hifadhi ni changamoto kubwa, mbinu ambazo tunaweza kuzitumia nje ya hifadhi hatuwezi kuzitumia ndani ya hifadhi, kulingana na sheria za uhifadhi, katika eneo la ndani ya hifadhi hatuwezi kupulizia dawa ni mambo yasiyoruhusiwa, sasa Mwananchi anapokuwa pale analiletea pia Taifa changamoto kubwa ya namna ya kuendelea kumuhudia wakati yupo kwenye eneo ambalo lina vikwazo vingi katika masuala ya huduma za Afya na za Kijamii.

Wengine watashangaa kwamba kwa nini haya magonjwa tunayataja sana kwa Ngorogoro, maeneo mengine pia yapo lakini Ngorongoro ni eneo ambalo hawa wananchi wapo katika maeneo ambayo yamejitenga kuwafikia katika maeneo yao ni changamoto sana, kwa hiyo ule ugumu wa kuwapa huduma unawafanya waendelee kuteseka na magonjwa ambayo yanathibitika ni magonjwa ambayo tunaweza kuyakinga na kuyaondoa, tunaona Wananchi wanaishi katika hifadhi ya Ngorongoro lakini ukienda Mataifa mengine huwezi kukuta Wanadamu wanaishi katikati ya Wanyama pori.

Magonjwa yapo sehemu nyingine lakini kiwango cha Magonjwa katika hifadhi ya Ngorongoro ni kikubwa, ukiangalia changamoto anazozipata Mtoto mdogo wa chini ya miaka mitano aliyeko Ngorongoro ni kubwa kuliko Mtoto aliyeko Dar- es Salaam, Mwanza, Morogoro na sehemu nyingine, kwa mtu yeyote anayedhamini na kuheshimu ubinadamu kama angeweza kutembelea yale maboma na kuona maisha wanayoishi hawa watoto wadogo, hawana hata uhuru wa kucheza kwa sababu akisogea mita 5 tu anaweza kupitiwa na fisi, chui, Simba na wanyama wengine wakali yani hawa ni Watanzania wenzetu ambao wapo kwenye mazingira magumu na ya kutisha kwa mtu yeyote mwenye moyo wa huruma atafikiria tofauti’’.

Profesa Hamis ameseyasema hayo wakati alipokuwa katika  Mkutano wa mtandao wa Zoom, akizungumzia kuhusu awamu ya pili ya uhamishaji wananchi katika Hifadhi ya Ngorongoro

**HABARI HII KWA HISANI YA GILLY BONNY*****


DKT. FREDY TUTAWARUHUSU WATU KWENDA POPOTE

"Awamu ya pili ya Uhamishaji Wananchi katika hifadhi ya Ngorongoro, tutahakikisha tunaruhusu watu wanaotaka kwenda sehemu nyingine nje ya Msomera waende, lakini tutakuwa makini kwa sababu tusije tukatatua matatizo ya Ngorongoro tukayapeleka sehemu nyingine, wakati watu wanavyojiandikisha kuhama tutataka kujua wanataka kwenda wapi? na tuweke utaratibu mzuri wa kwenda na kumpokelewa vizuri na kuweka takwimu vizuri ili waende sehemu ambayo inafaa’’ Hayo yamebanishwa na Dkt. Fredy Manongi Kamishna Mkuu Hifadhi ya Ngorongoro

RAIS DK.SAMIA SULUHU HASSAN, MAOFISA PUMA ENERGY WAFANYA MAZUNGUMZO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu  akizungumza na maofisa kutoka Puma Energy ambao ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Puma Energy kutoka kulia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Puma Energy ( Global)Hadi Hallouche, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Puma Afrika,  Fadi Mitri na Mkuu wa Puma Energy Afrika Constantin De Bartha



RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy na Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Mafuta ya Trafigura Hadi Hallouche (kulia kwa Rais Samia). Wanaofuata kulia kwa Rais ni Mkuu wa kampuni hiyo Afrika Constantin De Bartha, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Puma Afrika Fadi Mitri, Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu (kushoto kwa Rais) na Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzamia Fatma Abdallah.



Thursday 17 August 2023

KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM YA TAIFA.




Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 17 Agosti 2023 ameongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.





Monday 14 August 2023

WANANCHI WILAYA YA NGORONGORO WAANDAMANA KWA MABANGO KUSHINIKIZA WAHAMIE MSOMERA




Baadhi ya wananchi wanaoishi ndani ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wamepaza sauti zao kupitia vyombo vya habari wakiwa na Mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali.

Wananchi hao wakiongozwa na kiongozi wa Kimila wa jamii ya Wamasai Laigwanani Petro Tengesi wamefanya maandamano ya amani katika kijiji cha Kapenjiro wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kuchukizwa na wanaopinga wao kuhamia Msomera.
Wamesema wapo tayari kuhama muda wowote na kwamba wameshafika katika eneo la Msomera kujionea hali ilivyo na kwamba wameridhishwa nayo.
Kiongozi huyo wa mila amesema wamechoka kuishi eneo la Ngorongoro kwa kuwa hawana uhuru wa kufanya shughuli yoyote ya maendeleo kikiwemo kilimo ambacho kingewawezesha kupata chakula.




Sunday 13 August 2023

WANANCHI NGORONGORO WAOMBA KUHAMISHWA.



Baadhi ya Wananchi waliosalia ndani ya mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro (NCAA) wamewaambia Waandishi wa Habari kuwa wanaishi katika maisha ya tabu yasiyokuwa na huduma za kijamii na kwamba wanatamani kuondoka.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika kata za Nainokanoka na Naiyobi, wameeleza kuwa wanataka kuondoka kwa hiari kuwafuata wenzao katika makazi mapya ya Msomera huku wakiiomba serikali ya rais Samia ifanye hivyo haraka kwa kuwa hawaoni sababu ya kuendelea kuishi katika maeneo hayo.

Sinyati Emmanuel na Marry Kesumo Wanasema hawawezi kuishi mahali ambapo hakuna bara bara nzuri, maji,hospitali wala usafiri na kwamba hawana shughuli za maendeleo wanazozifanya kwa kuwa hawaruhusiwi hata kulima katika maeneo hayo.

Naye Jennifer Yuda kutoka kijiji cha Kapenjiro kata ya Naiyobi ambaye yupo tayari kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro kwenda Msomera, ameiomba serikali iwapatie maeneo kutokana na idadi ya Wake waliopo katika Boma husika.

Mosses Lenara ameishukuru Serikali kwa upendeleo ilioutoa kwao kwa kuwajengea nyumba Msomera na kuwapatia maeneo ya kilimo na ufugaji.

Serikali ilitoa nafasi ya kuwahudumia kila kitu ikiwa ni pamoja na kuwajengea Nyumba, Shamba na maeneo ya malisho, kuwasafirisha wao, mifugo na mizigo yao wote waliokubali kuhamia Msomera mkoani Tanga kwa hiari ili kupisha eneo hilo ambalo ni makazi ya wanyamapori wanaoingizia nchi mapato kupitia watalii.

Monday 7 August 2023

RAFIKI YAKO NI FOOD POINT



 

Thursday 3 August 2023

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT MPANGO AZINDUA MPANGO WA TATU WA TAIFA WA HUDUMA JUMUISHI ZA FEDHA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba akieleza juu ya makundi mbalimbali yaliolengwa kufikiwa na Mpango wa tatu wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023-2028 wakati alipowasili katika ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuzindua mpango huo leo tarehe 03 Agosti 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023-2028, hafla iliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Agosti 2023.







Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea kitabu cha Mpango wa tatu wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023-2028 kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba mara baada ya kuzindua mpango huo katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Agosti 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akionesha kitabu cha Mpango wa tatu wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023-2028 mara baada ya kuzindua mpango huo katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Agosti 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Fedha mara baada ya kuzindua Mpango wa Tatu wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023-2028, hafla iliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania  Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Agosti 2023. (waliokaa kutoka kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Wiebe de Boer na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema huduma jumuishi za fedha ni miongoni mwa vipaumbele vya Nchi pia ni lengo muhimu la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.

 Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua Mpango wa Tatu wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023-2028, hafla iliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam. Amesema huduma jumuishi za fedha ni nguzo muhimu inayopaswa kuzingatiwa kwa kuhakikisha watu wa makundi yote wanafikiwa.

 Makamu wa Rais ametoa wito kwa wataalam na wadau wa huduma jumuishi za fedha kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha wanaongeza kasi ya upatikanaji wa vitambulisho vya taifa ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha hususani kwa vijana. Aidha amewasihi watalaam hao kuhakikisha malengo yaliowekwa katika mpango huo wa tatu wa huduma jumuishi za fedha yanafikiwa kikamilifu ifikapo mwaka 2028 hususani kwa kuelekeza juhudi katika makundi ambayo hayajafikiwa ikiwemo watu wenye ulemavu, wakulima wadogo, wavuvi, vijana, wanawake na wafanyabiashara wadogo.

 Halikadhalika Makamu wa Rais amesema ni vema kuendelea na jitihada za kuimarisha ulinzi wa watumiaji wa huduma za kifedha dhidi ya uhalifu wa mtandaoni ili kuwajengea wateja imani ya kuendelea kutumia huduma hizo. Pia ametoa rai ya kupunguzwa kwa gharama za kutumia huduma rasmi za kifedha pamoja na kuongeza wigo wa dhamana ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo.

Makamu wa Rais ametoa wito wa kuongezwa na kurahisishwa kwa miundombinu ya malipo ya pamoja ili kuchochea matumizi ya huduma rasmi za fedha. Aidha amesema ni muhimu kuhakikisha upatikanaji wa mawasiliano kwa wote ili kupunguza matumizi ya fedha taslimu.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amesema Mpango wa Tatu wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha umeandaliwa kwa lengo la kuunganisha sekta binafsi na serikali ili kutatua changamoto za huduma jumuishi za fedha. Amesema mpango huo utasaidia kuongeza uelewa wa masuala ya huduma za fedha na kuongeza matumizi ya simu janja sambamba na kuhakikisha usalama wa wateja.

Wednesday 2 August 2023

KINANA -SHINA LA MUWA LINALOZALISHA VIKONYO KILA KUCHWAPO.







 MAKALA MAALUM-ZIARA YA KINANA

NA SAID MAKALA

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM  Abdulrhamani Kinana hivi karibuni aliihitimisha ziara yake ya ya siku 10 katika mikoa mitano,ziara ambayo ilikuwa mahususi katika utelezaji wa Ilani ya Chama hicho tawala cha CCM.

Katika Mikoa hiyo Kanali huyo mstaafu alizungumza mambo mengi kwa wanachi waiofurika katika mikutano yake ya hadhara lakini mengi  yakiwa yamejaa utamu wa chakula cha akili kama  mfano wa muwa uliojaa maji mengi na mtamu mithili ya asali , huku ukitafsirika kuwa na vikonyo kede kede shinani.

Katika ziara hiyo niliambatana naye niliona mengi ya kujifunza kutoka kwa Mwansiasa huyu nguli ambaye ama hakika ni wa kupigiwa mfano , katika ziara zake hizi si mara ya kwanza kuhuhudhuria huwa naburudika na maneno yake ya hekima yaliyojaa matumaini na hamasa ya kufufua fikra ambazo zilianza kufa kw awananchi ambao pengine katika maendeleo yao ya kiuchumi wanakutana na changamoto kadha wa kadha.

Akiwa Butiama Mkoani Mara nilimshuhudia kwa mara nyingine mzee Kinana akitoa tafsiri kubwa ya kuwaenzi mashujaa ambao wameipambania Tanzania katika kuleta ukombozi kutoka kwa Taifa jirani la Uganda, nakumbuka maneno haya aliyasema hivi

"Tuendelee  kuwaenzi mashujaa walioshiriki katika vita vya ukombozi dhidi ya nduli Idd Amin na shujaa wa kwanza ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye atabaki kuwa kielelezo wa Taifa la Tanzania"

Maneno hayo yalinikumbusha  maneno ya hekima na Buasara wakati Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini ambaye alichaguliwa kidemokrasia na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, ambaye alifariki Desemba 5, 2013 akiwa na umri wa miaka 95.

 Mandela anatambuliwa na taifa la Afika Kusini kwa kuleta mapinduzi ya Kiasisa kwani aliwahi kufungwa kwa kutumikia kifungo kwa miaka 27 kwa sababu ya mapambano yake dhidi ya mfumo wa kibaguzi wa Afrika Kusini unaofahamika kama  Ukaburu. Aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 1990, na kuwa rais miaka minne baadae, na kuachia madaraka baada ya kutumikia kwa kipindi kimoja tu, kitendo adimu kufanywa na wenye madaraka barani Afrika.

Akiwa mtu anayependwa duniani kote, Mandela alikuwa na namna ya mvuto katika maneno yake, Moja ya nukuu zake inatoka katika hotuba yake ya kijeuri aliyoitoa mahakamani wakati wa  kesi maarufu ya Uhaini ya Rivonia  mwaka 1964, ambapo. alisema "Nimepigana dhidi ya mfumo wa utawala unaowapendelea makaburu, na nimepigana dhidi ya mfumo wa utawala unaowapendela weusi. Nimekuwa na ndoto ya jamii ya kidemokrasia na huru ambayo watu wote wanaishi pamoja kwa mshikamano na fursa sawa. Ni ndoto ambayo nataraji kuiishi na kuitimiza. Lakini, kama itahitajika, hiyo ni ndoto ambayo nimejiandaa kupoteza maisha yangu kwa ajili yake."

Ukiacha hotuba hiyo ya kesi yake ya Rivonia, Mandela anaacha nyuma yake nukuu nyingi za kukumbukwa zenye busara alizozitoa katika kipindi chake chote cha uhai wake. Pamoja na kutuacha, anaendelea kuzungumza na ulimwengu kupitia watumiaji wa twita, ambao waliitikia habari za kifo chake kwa kusambaza maneno yake.

Maneno hayo ni ninayakumbuka sana kwa kuwa Mzee Kinana anendelea kutukumbusha na yeye ni mmoja wa watu wenye msimamo wa kusimamia maneno yenye Busara mtu ambaye hapendi kukwezwa, hata wasaidizi wake wanatambua hilo lakini mtu ambaye anatamani kuona mtanzania anapata haki ya kujenga historia bora ya kiuchumi.

Kinana, katika kauli zake akiwa Mkoani Mara kwenye mwendelezo wa ziara zake alitumia wasaa mwingi kutoa nasaha kwa watanzania kama alivyokumbusha watanzania kuthamini tarehe ya Julai 25 kuwaenzi Mashujaa .

Lakini katika hautua nyingine ambayo Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana katika ziara zake hizi akiwahutubia wanachi katika maeneo mbalimbali alifurahisha umma na wengine wakisema pembeni 'Huyu mzee jamani amebarikiwa kipawa cha kuongea" na maeneo hayo yalitoka pale alipowataka watanzania kuweka imani kwa Mhe. Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Sukuhu Hassan  katika harakati zake za kuleta maendeleo nchini hususani kuwashawishi wawekezaji wakubwa kuja nchini kuwekeza.

Kauli hiyo akiibainisha katika Mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Mkendo Musoma mjini Mkoani Mara akitumia muda mfupi lakini wenye maneno yaliyojaa busara , ambapo pia hakuacha kuzungumzia masuala mazima ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.

"  Kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira mazuri na kutoa  furusa ya kujiajiri kwa wananchi wake na kufanya kazi zao bila usumbufu wowote kwa kuwa huru zaidi wasikutane na changamoto katika kazi zao,ndio maana tupo katika ziara kuangalia CCM, imefanya nini,tupeni imani sisi CCM, kazi yetu ni kuleta maendeleo na si vinginevyo"Alisema Kinana...

MAKALA HII ITAENDELEA.....KUANGAZIA ZIARA YA MZEE KINANA...NA MAFAKIO YAKE.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube