Yanga itashuka dimbani kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba na Rayon huku ikiwa haina nafasi yoyote ya kusonga mbele.
Kwa mujibu wa Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, amesema wachezaji wote wako vizuri kiafya na hakuna yoyote ambaye yuko majeruhi.
Saleh ameeleza lengo lao kubwa kwenye kipute hicho ni kuweka heshima ya kuhakikisha wanapata matokeo licha ya kuwa hawana nafasi ya kusonga mbele.
Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki ambapo itachezwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo uliopo jijini Kigali.
Yanga ilianza michuano hiyo kwa kusua sua baada ya kukubali vipigo vikubwa viwili, wakati ilipokutana na USM Alger ya Algeria nchini Algeria na kuchapwa mabao 4-0 na Gor Mahia kuwachapa idadi kama hiyo.
Timu hiyo ilijitutumua ilipocheza Dar es Salaam, na USM Alger baada ya kuifunga timu hiyo mabao 2-1
No comments:
Post a Comment