Mshambuliaji Alexandre Lacazette akishangilia baada ya kuifugia Arsenal bao la kusawazisha dakika ya 90 na ushei ikitoa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa kirafiki wa Kombe la Mabingwa wa Kimataifa Uwanja wa Aviva mjini Dublin kufuatia Antonio Rudiger kuanza kuifungia The Blues dakika ya tano. Arsenal ikaenda kushinda kwa penalti 6-5 kufuatia Ruben Loftus-Cheek kukosa penalti ya mwisho ya Chelsea na Alex Iwobi kufunga kwa upande wa Washika Bunduki wa London, ambao wapo chini ya kocha mpya, Mspaniola, Unai Emery aliyechukua nafaisi ya Mfaransa, Arsene Wenger mwezi uliopita. Waliofunga penalti za Arsenal ni Alexandre Lacazette, Reiss Nelson, Matteo Guendouzi, Ainsley Maitland-Niles, Mesut Ozil na Alex Iwobi wakati za Chelsea zimefungwa na Danny Drinkwater, Tammy Abraham, Victory Moses, Emerson na Lucas Piazon |
No comments:
Post a Comment