BREAKING

Tuesday, 7 August 2018

DSTV WAIREJESHA LIGI YA ITALIA -SERIE A SASA WATEJA WAKE KUSHUHUDIA LIGI KUBWA ULIMWENGUNI KWA BEI 'KIDUCHU'

Baada ya kiu ya muda mrefu, sasa wateja wa DStv wataanza tena kushuhudia moja ya ligi maarufu kabisa duniani – Ligi ya Italia – Serie A sasa MultiChoice imetangaza habari njema kuwa kuanzia msimu huu, ligi hiyo itaonyeshwa mubashara kupitia DStv.
 
Mbali na Serie A ambapo atakuwepo nguli wa soka Cristiano Ronaldo, wateja wa DStv wataendelea kufurahia ligi na michuano mikubwa mingi duniani ikiwemo Ligi ya Uingereza (Premier League) na La Liga.
 

Mbali na habari za kurudi kwa Serie A, DStv pia itaongeza maudhui zaidi katika soka msimu huu. Watumiaji wa DStv Bomba, wataweza kuona zaidi ya mechi 100 katika michuano ya  Serie A na Ligi Kuu ya Uingereza, huku wateja wa DStv Family wao watakuwa wakipata mechi zote 380 za michuano ya Serie A na mechi zaidi ya 120 kutoka Ligi Kuu ya Uingereza. Watumiaji wa kifurushi cha DStv Compact, Compact Plus na wateja wa Premium watakuwa na upatikanaji wa mechi zote za Premium League, Serie A na mechi zote 380 za La Liga.

Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo (Kushoto) na Meneja Masoko Alpha Mria (Kulia) wakiwa na wachezaji wakongwe wa soka hapa nchini muda mfupi baada ya uzinduzi wa msimu wa soka ambapo DStv imetangaza kurejea kwa ligi ya Italia Serie A.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa soka,, Meneja uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo alisema wateja wa DStv watapata fursa ya kufurahia  msimu huu mpya wa soka na katika kunogesha zaidi amesema michuano ya ligi ya uingereza itatangazwa kwa lugha ya kiswahili.

Amesema pia huduma ya DStv Now ambayo inamuwezesha mteja kutazama DStv popote alipo itawafanya watanzania wengi kufurahia msimu huu wa soka kwani unachotakiwa tu ni kuwa na akaunti yako ya DStv na unaweza kutazama katika vifaa zaidi ya vinne kama vile simu, kompyuta, na televisheni ya kawaida.

3

Watangazaji maarufu wa Soka hapa nchini (kutoka kushoto) Maulid Kitenge, Aboubakar Liongo, Edo Kumwembe na Ephraem Kibonde wakiwa katika uzinduzi wa msimu mpya wa soka watangazaji hao watakuwa wakiwaletea matangazo ya ligi kuu ya uingereza msimu huu kwa kiswahili.
 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube