Kikosi cha Manchester United kimeanza harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2018/19 kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester City.
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Old Trafford, United imejipatia mabao yake kupitia kwa Paul Pogba aliyefunga kwa njia ya penati pamoja na Luke Shaw.
Bao pekee la Leicester limewekwa kimiani na Jammie Vardy aliyefunga kwa njia penati mnano dakika za mwisho.
Matokeo hayo yanifanya United kuwa kileleni kwa muda huku mitanange mingine ikisubiriwa kuendelea wikiendi hii.
No comments:
Post a Comment