Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imepangua ratiba ya mechi za mwanzo zilizopangwa kuanza Agosti 22.
Upanguaji wa ratiba hiyo umekuja kutokana na changamoto ya ambapo serikali imetoa taarifa kuwa Uwanja huo hautotumika kuanzia Agosti 22 mpaka Septemba Mosi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amesema hatua hiyo imekuja kufuatia serikali kuwatumia barua wakieleza kuwa kiwanja hicho hakitoweza kutumika.
Kutokana na maamuzi ya serikali, Wambura amesema mechi ambazo zilipaswa kuanza siku hiyo ndani ya Uwanja wa taifa baina ya Simba vs Tanzania Prisons, Mwadui na Mbeya City zitahamishiwa Uwanja wa Uhuru.
Kwa maana hiyo Simba na Tanzania Prisons sasa watachezea Uwanja wa Uhuru huku mchezo wa Mtibwa uliopangwa kuchezwa Agosti 23 huku Yanga wkiwa wenyeji, utapigwa Uwanja wa Uhuru badala ya Jamhuri Morogoro.
Simba pia ambayo ilipaswa kukipiga na Lipuli katika Uwanja wa Taifa, sasa itakuwa tofauti tena na badala yake utachezewa kwenye dimba la Uhuru mnano Septemba 2 kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa na shughuli zingine.
No comments:
Post a Comment