BREAKING

Saturday, 2 September 2017

NI MSUVA NA BOTSWA,UWANJA WA UHURU APIGA MABAO YA KIDEO......



Mabao  mawili ya winga mpya wa klabu ya Difaa Hassan El- Jadida yameipa Tanzania ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Msuva aliyejiunga na timu ya Ligi Kuu ya Morocco mwezi uliopita alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya The Zebras na amefunga bao moja kila kipindi, Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Elly Sasii aliyesaidiwa na Soud Lila na Frank wote wa Tanzania, hadi mapumziko Taifa Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Simon Msuva alipokea pasi ndefu ya kiungo Hamisi Abdallah wa Sony Sugar ya Kenya,  na kumpasia kiungo wa Simba, Muzamil Yassin kabla ya kuingia nayo kwenye boksi kwa kasi na kufumua shuti kali lililompita kipa wa The Zebras, Mwambule Masule dakika ya sita.

Katika kipindi hicho, ilishuhudiwa Taifa Stars wakicheza vizuri zaidi na kutengeneza nafasi chache za kufunga, ambazo hata hivyo walimudu kuitumia vizuri nafasi moja tu kupata bao.

The Zebras nao hawakuwa hawakuwa nyuma kushambulia kwani walipeleka mashambulizi langoni mwa Taifa Stars na kukaribia kufunga mara mbili kama si uhodari wa kipa wa Simba, Aishi Salum Manula.

Kipindi cha pili, Zebras walirudi kwa nguvu na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Taifa Stars, lakini safu ya ulinzi ikiongozwa na mkongwe Kevin Yondan ilikuwa imara kudhibiti hatari zote. 

Nahodha, Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji alicheza vizuri pamoja na kudhibitiwa vikali , sambamba na nyota huyo pia Kiungo wa Tenerife ya Hispania, Farid Mussa na mshambuliaji wa Dhofar ya Oman Elius Maguli wote waliingia kipindi cha pili na wakacheza vizuri 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube