BREAKING

Wednesday, 27 September 2017

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA

Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Kulia) akizungumza jambo na Mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu mara baada ya kuwasili mkoani singida tayari kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Mwenye suti nyeusi) akielekea kujionea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni, kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe Daniel Mtuk.
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe alipotembelea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akizungumza jambo mara baada ya kutembelea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akikagua ujenzi wa eneo maalamu litakalotumika kwa ajili ya kuhifadhi umeme kwa ajili ya kusafirisha maji kuelekea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Manyoni katika eneo la Mitoo.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza jambo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe kukagua utekelezaji wa ilani uchaguzi ya CCM 2015-2020
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akisisitiza jambo mbele ya wananchi, Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Kulia) akisalimiana na wananchi wa Kitongoji cha Kaloleni mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kujionea hali ya upatikanaji wa maji.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe Daniel Mtuka (Kulia) akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya vyanzo vya maji.
Mfereji wa Skimu ya Umwagiliaji kijijini Itagata ukiwa katika hatua nzuri za ujenzi
Bwala la Skimu ya Umwagiliaji lililogomewa na wananchi wa kijiji cha Itagata mara baada ya kubaini kuwa linavuja kutokana na mashimo yaliyopo yanayopelekea upotevu wa maji.

Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Itagata, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kuhusu namna bora ya kukamilisha Mradi wa Ujenzi wa Bwala la Skimu ya Umwagiliaji.


Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe ameanza ziara ya kikazi Mkoani Singida ambapo atatembelea na kukagua Miradi ya Maji na vyanzo vya uboreshaji upatikanaji wa maji.

Naibu Waziri Mhe Kamwelwe amepokelewa na Mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Ambaye Ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni.

Mara Baada ya mapokezi hayo Mhe Naibu Waziri alianza shughuli ya kukagua Mradi wa chanzo cha maji Kintinku/Lusilile ambapo amewasihi wananchi kutunza mazingira hususani misitu ya asili kwani ndio chanzo cha upatikanaji wa maji.

Mhe Kamwelwe ameelekeza wananchi kulinda na kutunza vyanzo vya maji Sambamba na kutoa taarifa za uharibifu wa vyanzo vya maji na ukataji ovyo wa miti na uharibifu wa mazingira.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kufikia Mwaka 2020 wananchi waweze kupata maji kwa urahisi katika maeneo wanayoishi tofauti na hali ya upatikanaji wa maji kwa hivi Sasa kwa wananchi wanaotumia umbali mrefu kutafuta maji.

Aliwasihi wananchi kuvitunza vyanzo hivyo vya maji kwani pindi vitakapoanza kufanya kazi vitapunguza ukali wa uhaba wa upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Manyoni na Mkoa wa Singida kwa ujumla.

Alisema kuwa katika Bajeti ya kipindi Cha mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Vijijini imetengewa shilingi Milioni 611 huku eneo la Mamlaka ya Mji wa Manyoni ikiwa imetengewa zaidi ya Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya upatikanaji wa maji utakaopelekea Wilaya ya Manyoni kufikia 50% ya upatikanaji wa maji.

Mhe Kamwelwe aliwataka wakurugenzi kutekeleza miradi mbalimbali katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa ukarabati wa miradi ya maji, Uchimbaji wa visima virefu, na Ukarabati wa pampu zinazotumia upepo (Windmill).

Sambamba na hayo pia Mhe Naibu Waziri alikiri kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazosababisha kutopatikana kwa maji ya kutosha ambapo ameahidi kuzifanyia kazi kwa haraka ambazo Ni pamoja na uchakavu wa miundombinu ya mabomba hasa eneo la usambazaji, Taasisi nyingi za serikali kutolipa Ankara zao za za maji, Kupandana kwa gharama za uendeshaji na Mamlaka kutokuwa na vyanzo vyake vya fedha.

Akiwa Kijijini Itagata, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Bwawa na Skimu ya Umwagiliaji, Mhe Naibu Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe aliagiza Uongozi wa Umwagiliaji Kanda ya Kati Dodoma kufika Mjini Singida ndani ya siku mbili ili kubaini changamoto ya kukwama kwa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Itagata lililokataliwa na wananchi kutokana na kuvuja kwake mnamo Septemba 2015 mara Baada ya kukamilika.

Mradi wa Ujenzi wa Bwala la Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji Cha Itagata ukikamilika utaweza kuhudumia Hekta zipatazo 160 katika eneo tambarare kwa ajili ya Kilimo Cha Umwagiliaji hususani zao la mpunga, Mazao ya Bustani na Vitalu vya kuoteshea Miche ya Tumbaku kwani eneo Hilo Lina udongo rafiki kwa Kilimo hicho.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube