BREAKING

Monday, 4 September 2017

DANNY MRWANDA JEURI SANA, ASEMA SOKA BET WAMEWATIA NJAA YA MAFANIKIO SASA....NI BAADA YA KUPATA UDHAMINI MNONO.

Danny Mrwanda akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajiliya kusaini mktaba wa udhamini,Kati ya Maji Maji na Soka Bet.

Mshambuliji wa Kimataifa aliyewahi kutamba pia na timu ya Taifa ya Tanzania ambaye kwa sasa anaitumikia timu ya MajiMaji ya Songea Danny Mrwanda, ametamba kwamba baada ya klabu yao kupata udhamini mnono wa milioni 150, kutoka Soka Bet sasa wao ni kucheza Kandanda ili kupata matokeo.

Kauli hiyo ameitoa wakati viongozi wa klabu yake walivyokuwa wakisainiana mkataba wa kudhamini klabu yao kwa mwaka mmoja ,ambapo mekiri sasa ,kazi iliyobaki ni kusakata kandanda pekee Uwanjani.

Nyota huyo aliyewahi kung'ara zaidi kimataifa ,amesema kikosi cha Maji Maji msimu huu kimeandaliwa vyema na wapo katika kuhakikisha wanapambana katika,Ligi Kuu ya Tanzania Bara hadi kieleweke.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube