Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu MICHAEL LUWONGO, akiwana wachezaji wa Timu ya Tanzania ya wanawake inayoondoka kesho kuelekea Uganda
Kikosi cha wachezaji Kumi na tatu kinachounda timu ya Tanzania inayokwenda nchini Uganda kushiriki mashindano ya Afrika kimeagwa kwa ajili ya kwenda kushiriki michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Septemba saba hadi tisa jijini Kampala.
Wachezaji hao ni Sophia Virgo, Sarah Dennis, Sophia Mathias, Angel Eaton, Hawa Wanyenche, Vicky Elias, Tayana William, Mwanaidi Ally na Habiba Juma.
Wengine ni Aine Magombe, Habiba Sanze, Chiku Elias, na Sheridan Chilipati.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika kambi yao ya mazoezi kwenye viwanja vya Lugalo, licha ya kuridhishwa na namna walivyojiandaa, wachezaji hao wameeleza kiu ya ushindi waliyonayo na hivyo wakiahidi vikombe.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu MICHAEL LUWONGO, amewashukuru wadau wote waliojitokeza kusaidia kambi ya maandalizi, huku akiwataka wachezaji kujitahidi kwani si tu watajipatia zawadi lakini pia watailetea sifa nchi.
No comments:
Post a Comment