Balozi wa Mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 80 Mshimdi Mkuu wa Mchezo huo, Rashid Ally katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Regence Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Lumuliko Mengele, akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni mama wa mshindi huyo, Fatma Kavila. Katikati ni mshindi, Rashid Ally.
Wapiga picha kutoka vyombo vya habari wakichukua tukio hilo.
Meza kuu. Kutoka kulia ni Maneja Masoko kutoka Commercial Bank Of Africa (CBA), Solomon Kawiche. Baba wa mshindi huyo, Kamba Kavila, Meneja Masoko wa Kampuni ya The Network Product Tatu Mzuka, Lumuliko Mengele, Rashid Ally na mama yake Fatma Kavila.
Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed, akizungumza katika hafla hiyo ya kumkabidhi mshindi huyo kitita hicho.Rashid Ally akizungumza na wanahabari kuhusu ushindi wake.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Maneja Masoko kutoka Commercial Bank Of Africa (CBA), Solomon Kawiche, akizungumza jinsi watakavyomsaidia mshindi huyo jinsi ya kutumia fedha hizo.
Baba, mama na mwana wakiwa wameshika mfano wa hundi wa kiasi hicho cha fedha alichoshinda mtoto wao.
MSHINDI Mkuu wa mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka , Rashid Ally, leo amekabidhiwa sh.milinoni 80 alizojishindia katika droo kubwa iliyochezwa Jumapili.
Rashid ambaye alijishindia kiasi hicho cha fedha katika mchezo huo wa Tatu Mzuka, alionyesha kutoamini, huku akiwa na furaha na shukrani baada ya ushindi huo wa kihistoria. Rashid, ambaye ana umri wa miaka 21 tu, anaishi na familia yake maeneo ya Temeke, Dar es Salaam.
Akizungumzia ushindi wake, Rashid ambaye amemaliza kidato cha nne hivi karibuni, alisema kuwa alikuwa anacheza angalau mara 4 hadi 6 kwa wiki kwa kutumia pesa aliyokuwa anaipata katika shughuli zake za kila siku.
'Ndoto yangu ni kujenga nyumba, na kuwekeza katika kilimo, kitu ambacho nitafanya kwa kushirikiana na mama pamoja na Baba yangu. Nia yangu ni kuikuza iwe ni biashara kubwa ' alisema Rashid.
Pia alisema ana mpango wa kuendelea kucheza mchezo na kuwa balozi wa Tatu Mzuka, ili kuwasaidia watu kufurahia mchezo huo na kuuamini.
"Watu wengine ni wagumu kuamini kwamba unaweza kushinda kiwango hiki kikubwa cha fedha kupitia shilingi 500 tu. Ninafurahi kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuthibitisha hili"
Balozi wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein, alisema Tatu Mzuka ina nia ya kuendelea kutengeneza washindi zaidi wa zawadi ambazo zitabadilisha maisha ya watu na familia zao.
"Kama Tatu Mzuka, tunafurahi kuona kwamba mchezo huu unabadilisha maisha ya Watanzania. Mbali na kiwango kikubwa cha pesa tunachokitoa katika droo kubwa ya kila Jumapili, tumeishalipa zaidi ya milioni 350 kama ushindi wa kila siku kwa wachezaji mbalimbali wa mchezo wetu. Kwa wastani mtu mmoja anakuwa mshindi wa Tatu Mzuka kila sekunde 10, masaa 24 kwa siku, na siku 7 kwa wiki "alisema Mussa.
Pia akizungumza katika tukio la kukabidhi ushindi huo, Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed alimpongeza Rashid kwa ushindi huo na akamwomba kuwekeza fedha kwa makini ili abadilishe maisha ya watu wengine. Hemed aliipongeza Kampuni ya The Network Product Tatu Mzuka kwa kuendesha mchezo kwa uaminifu na kwa haki na kutimiza ahadi yake kwa umma.
No comments:
Post a Comment