BREAKING

Thursday, 28 September 2017

YANGA WANAJIFUA ZAIDI YA SAA TATU, WANAJIWINDA NA MTIBWA SUGAR -LIGI KUU TANZANIA BARA










Na Said Makala

Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wameendelea kujiweka sawa kwa ajili mechi ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar,Jumamosi wakifanya mazoezi yao katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam..

Channel ten imewashuhudia wachezaji hao katika Mazoezi hayo wakiwa chini ya Kocha George Lwandamina pamojan na wasaidizi wake Shadrack Nsajigwa na Juma Pondamali.

Kikosi cha Yanga kimecheza mechi nne na kushinda mbili, sare mbili,hivyo kimejikusanyia pointi nane sawa na watani wao Simba, hivyo watahakikisha wanashinda katika mchezo wao ujao ili kujiweka kileleni mwa Ligi Kuu ya tanzania bara.

Kikosi hicho kitamkosa kiungo wao nyota Papy Tshishimbi katika mechi ijayo kutokana kuwa na adhamu ya kadi ya Kadi tau za njano na kuweka rekodi mbaya kwani ndani ya merchi nne amepata kadi tatu.

Kadi yake ya tatu alipigwa katika mechi dhidi ya Ndanda FC, mechi ambayo Yanga ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube