BREAKING

Friday, 30 June 2017

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA ,ASHUHUDIA MAGARI 103 YAKIWA NA SHEHENA YA MAHINDI NJIA PANDA YA HIMO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo Kamanda wa Polisi ,Hamis Issah na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba wakitembelea maeneo ambayo yameshikiliwa magari yaliyobeba shehena ya Mahindi .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizunbgumza na baadhi ya wafanyabaishara wa Mahindi ambao magari yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Wafanyabiashara ambao Mahindi yao yanashikiliwa katika eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipofika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitizama Malori yenye Shehena ya Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyuma ya vituo vya Mafuta .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiongozana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issa wakiodoka katika eneo hilo baada ya kuangalia malori yanayoshikiliwa yakiwa na shehena ya Mahindi.
Baadhi ya Magari yakiwa yameegeshwa katika maeneo tofauti tofauti yakiwa na shehena ya Mahindi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.


ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili mpakani mwa nchi jirani ya Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha Malori yanayosafirisha Nafaka kwenda nchi jirani ya Kenya.
Uchunguzi uliofanywa na Globu ya Jamii umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha Malori hayo ,mengine yakiwa na Matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika Magari Madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.
Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio  ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari  zilizopo katika  vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.
Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda kusiko julikana .
Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.
“Magari yetu yapo pale Sheli Maount Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi  Matandiboi wakapiga simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi ,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara Mariam.
Alisema alimuelewa Waziri Mkuu katika agizo lake kwamba magari yaliyopo mpakani ndio yashikiliwe  na si kama lilivyofanya jeshi la Polisi kukamata magari yaliyokuwa Njia Panda kuelekea Moshi na Arusha huku wakimuomba Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi  kwa wasaidizi wake juu ya agizo lake.
Mfanyabiashara Kanyota alisema amekuwa akifanya biashara ya kusafirisha mazao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi lakini anashangazwa na hatua ya kuzuiliwa kwa  Mahindi yake ambayo amekuwa akinunua na kuyauza katika viwanda vya kutengeneza unga kwa ajili ya Chakula.
“Tulikua tunaomba Mkuu wa mkoa ajue kwamba sisi ni wafanyabiashara tunaolipa kodi halali ya serikali atusaidie tufikishe mazao yetu sehemu yanapotakiwa kufika ,Mahindi yangu yanatoka Mbeya ,mkulima aiyeniletea mimi kama Dalali ametoka Tunduma.”alisema Kanyota.
Kauli ya Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro imepigiria msumari katika Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaifisha Mahindi pamoja na gari litakalokutwa kuanzia June 26 mwka huu likiwa limebeba na kusafirisha Mahindi kwenda nje  ya nchi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa alisema jana ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari kuwa magari 103 yaliyokamatwa Himo na Njia Panda yatahesabiwa kama sehemu ya uhujumu uchumi na kwamba yatataifishwa .
“Magari yaliyokamatwa kule Siha ,tayari tulikwisha amua kwamba yatapelekwa Nationa Milling(Ghala la chakula la taifa)  Arusha ,lakini haya ya Himo ,Waziri Mkuu Alisha agiza kwamba kuanzia tarehe 26 ,magari yote yatakayokamatwa ,Bidhaa pamoja na magari yenyewe yatahesabiwa kuwa ni sehemu ya uhujumu Uchumi ,kwa hiyo yatataifishwa.”alisema Mghwira.
Mghwira alisema baada ya mfululizo wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro juu swala zima la uuzaji na usafirishaji wa chakula nje ya nchi,kamati imefanyia kazi tamko la Waziri Mkuu kutaka kujiridhisha vya kutosha juu ya hali ya chakula iliyopo Kilimanjaro na mikoa ya jirani.
“Uogozi wa mkoa wa Kilimanjaro unapenda kuwatangazia wananchi wote,hususani Wafanyabiashara wa Sukari na Nafaka za Mpunga,Mchele ,Mahindi na Unga wa Mahindi ya kuwa ni marufuku kwa mfanyabiashara yoyote au mwananchi yoyote kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi bila kibali cha serikali”alisema Mkuu huyo wa Mkoa .
Alisema kukiuka agizo hilo ni kuhujumu uchumi wa nchi  kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 3 cha jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu Uchumi sura ya 200 ya sheria za Tanzania na pia ni kukiuka agizo la Waziri Mkuu,kupitia waraka wake alioutoa  Mei 30,2017,uliozuia utokaji  wa vyakula na sukari kwenda nchi jirani .
Alisema kwa kukiuka sheria hiyo kunaweza kusababisha upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini na kusababisha Mamlaka ya Mapato hapa nchini (TRA)  kukosa takwimu muhimu wa bidhaa zinazosafirishwa nje
“Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro imejiridhisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari  na nafaka hizo nyakati za usiku na hiki ndicho kinaleteleza kukosa takwimu muhimu kwa kupitia njia ambazo si rasmi kwa kushirikiana na baadhi ya askari polisi ambao sio waaminifu.
Wakati wa baraza la Idd lilifanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi,Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa alitangaza kupiga marufuku usafirishaji wa Mahindi kwenda nchi jirani na kwamba atakaye kiuka utaratibu huo atahukuliwa hatua kali za kisheria.
Mwisho.


Wednesday, 28 June 2017

WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO

Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .
Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.

Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari .

Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) ,Jonesia Rukyaa  kuchezesha mchezo huo  wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .

Saturday, 24 June 2017

SHUJAAZ WAWAFUNDA WAANDAAJI WA MASHINDANO YA EAST AFRICA CUP 2017

Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akitoa maelezo kwa washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na watayarishaji wa Mradi wa Shujaaz kwa ajili ya kutoa eimu juu ya maswala mbalimbali ikiwemo Ujasiliamali pamoja na Kilimo,Warsha ambayo inafanyika sambamba na Mashindano ya Kimataifa ya Vijana kwa vijana wa nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akitoa maelezo kwa washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi
Washiriki katika Warsha hiyo.
Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumalizika kwa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi
Baadhi ya Vijana waliofanikiwa kuingia katika Kijiji cha Shujaaz wakionesha umahiri wao katika uimbaji ambapo pia walipata zawadi kutoka Shujaaz.
Timu za watoto chini ya miaka 13 za Msimamo na Right to Play kutoka Dar es Salaam zikichuana katika mashindano ya East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Moshi Ufundi.
Vijana chini ya miaka 13 wakioneshana umahiri  katika kusakata soka katika mashindano ya East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika viwanja vya Moshi Technical.
Baadhi ya vijana wakifuatilia mchezo huo.
Katika Kijiji cha Shujaaz wakishiriki michezo mbalimbali ikiwemo ya kukimbia huku wakiwa ndani ya magunia.
Kijiji cha Shujaaz kimekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wanaoshiriki mashindano ya East Africa Cup 2017.

Thursday, 22 June 2017

MULTICHOICE TANZANIA YASAIDIA WATOTO YATIMA TANDALE

 Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo akikabidhi mashuka kwa Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam Kuruthum Juma (wa pili kulia). Wa pili Kushoto ni Malkia wa Taarabu Hadija Kopa na kulia ni  Muigizaji maarufu wa tamthilia ya Huba Riyama Ali ambao ni mabalozi maalum wa DStv. 

 Watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Almadinnah kilichopo Tandale wakipokea vyombo kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo baada ya kupokea msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kutoka kampuni hiyo jana.

Mshonaji katika mradi wa ushonaji wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah cha Tandale jijini Dar es Salaam Aziza Amri (wa pili kulia) akitoa maelezo kuhusu mradi huo unaofadhiliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania. Kutoka kushoto ni Malkia wa mipasho Hadija Kopa ambaye ni balozi maalum wa DStv, Bi Kuruthum Juma ambaye ni mkuu wa kituo hicho, Baraka Shelukindo Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania na kulia ni Muigizaji maarufu wa tamthilia ya Huba Riyama Ali.

RONALDO AING'ARISHA URENO KOMBE LA MABARA WENYEJI URUSI HOI

Cristiano Ronaldo akishangilia bao pekee dhidi ya wenyeji, Urusi katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mabara Uwanja wa Otkrytiye Arena mjini Moscow.KWA PICHA ZAIDI GONGA HAPA>>>>

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube