Cristian Ronaldo akishangilia moja ya mabao aliyofunga jana Bayern Munich |
Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya imeendelea usiku wa jana kwa kuchezwa michezo miwili.
Cristiano Ronaldo ameendelea kudhihirisha yeye ni hatari baada ya kupiga hat trick wakati Real Madrid ikiitwanga Bayern Munich kwa mabao 4-2 na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Madrid inakwenda nusu fainali kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Munich na yote mawili ya Madrid yalifungwa na Ronaldo.
Kwa mabao hayo, maana yake Ronaldo amefikisha mabao 103 aliyofunga katika michuano ya Ulaya ngazi ya klabu,kwani usiku wa jana aliingia uwanjani akiwa na mabao 100 baada ya kufunga mawili mjini Munich.
Bayern walianza kufunga bao la kwanza dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti kupitia Robetro Lewandowski, Madrid wakasawazisha dakika ya 76 akifunga Ronaldo kabla ya beki Sergio Ramos kujifunga dakika mbili baadaye.
Kipigo cha 2-1 kwa Madrid kilisababisha kuongezwa kwa dakika 30 na ndipo Madrid ilipoanza kuporomosha mvua ya mabao, Ronaldo akifunga dakika ya 106 kwa pasi ya Ramos na Marcelo akawachambua mabeki wanne kabla ya kumpa pasi safi Ronaldo aliyefunga bao la nne dakika ya 110.
Marco Asensio ndiye aliyefunga bao la nne katika dakika ya 112 na kumaliza kazi dhidi ya Bayern ambao walicheza pungufu kuanzia dakika ya 84 baada ya Arturo Vidal kupigwa kadi nyekundu.
No comments:
Post a Comment