Baada ya kipigo kutoka kwa wapinzani wake Barcelona, Madrid imeamka tena kwenye La Liga baada ya kuitwanga Derpotivo la Coruna kwa mabao 6-2, huku wapinzani wake waliowafunga Barcelona wao wakitoa kipigo cha hatari cha mabao 7-1 dhidi ya Osasuna.
Pamoja na kucheza bila ya Cristiano Ronaldo, Madrid imeiangushia Derpotivo kipigo hicho kikali ikiwa nyumbani.
James Rodrigues alifanikiwa kufunga mabao mawili huku Alvaro Morata, Lucas Vazquez, Isco na Casemiro kila mmoja akitupia bao moja na kutengeneza ushindi huo mkubwa wa ugenini.
Derpotivo nayo ilijitutumua na kupata mabao mawili kupitia Florin Andone na Joselu ingawa hayakusaidia kubadili matokeo ya kupata pointi tatu.
Barcelona wao waliichakza bila huruma timu ya Osasuna baada ya kuwapa kipigo cha aibu baada ya kupokea kipigo cha mabao 7-1
No comments:
Post a Comment