Fenerbehce ya Uturuki imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambulizi Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji ambako amekuwa aking'ara.
Kwa sasa, mkongwe Robon van Persie ndiye kiongozi wa ushambulizi katika timu hiyo ya pili kwa ukubwa nchini Uturuki baada ya Galatasaray.
Lakini Fenerbehce inaonekana imeamua kujiimarisha na sasa inasaka mshambulizi kijana na hatari, Samatta anatupiwa jicho.
Wengine ambao wanapewa nafasi ya kusajiliwa na Fenerbehce ni Thomas Bruns, Theo Bongoda na Ridgeciano Haps.
No comments:
Post a Comment