Nahodha wa Azam FC John Bocco akiwa na msaidizi wake Himid Mao wakionyesha baadhi ya makombe walioshinda, walipotembelea wadhamini wao Benki ya NMB |
Nahodha msaidizi wa Azam FC Himidi Mao akikabidhi kombe kwa Afisa Mkuu wa fedha wa Benki ya NMB |
Benki ya NMB imesema itaendelea kutoa udhamini wa muda mrefu kwa Mabingwa wa kombe la Kagame 2015/2016 timu ya Azam FC baada ya leo kufanya ziara katika Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo imefanya ziara fupi katika benki hiyo ya NMB na kukutana na wafanyakazi wa kila idara pamoja na kuonyesha vikombe vya ubingwa mbalimbali walivyopata katika mashindano tofauti.
Makombe ambayo walionyesha kwa uongozi wa NMB ni pamoja na kombe la Ubingwa wa CECAFA, kombe la Mapinduzi, kombe la timu ya vijana Afrika ,pamoja na kombe la Ngao ya Hisani.
Akizungumzia mahusiano mazuri kati ya timu ya Azam FC na NMB Afisa Mkuu wa fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas, amesema kuwa wataendelea kuboresha udhamini kwa timu hiyo kutokana na kiwango bora ambacho timu imekuwa ikikionyesha.
Kwa uapande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Saad Kawemba, amesema kuwa timu hiyo bado ina malengo makubwa zaidi ya mbeleni, hivyo amewahaidi wadhamini wao kuwa wataendelea kufanya vyema hususani kwenye michuano ya ndani ambayo itawapa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment