Kamati ya utendaji ya klabu ya soka ya Yanga imesema imepeleka ripoti TAKUKURU ya kuchunguzwa kwa kamati ya masaa 72 ya TFF,Juu ya rufaa ya klabu ya soka ya Simba ambayo imemkatia mchezaji wa kagera Sugar Faki Faki,ambaye Simba wanadai mchezaji huyo alichezeshwa akiwa na kadi za njano tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga Salum Mkemi amesema kuwa hawana imani na kamati hiyo kwa kuwa inaonyesha kuwa na chembe chembe ya rushwa,ambayo inataka kuipa simba pointi tatu kutoka kwa Kagera,ambao waliifunga Simba mabao 2-1.
Aidha Mkemi ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa iwapo Simba watapewa pointing hizo za mezani watachukua hatua Kali kama klabu.
No comments:
Post a Comment