Mwanariadha pekee wa Tanzania anayetarajiwa kushiriki mashindano ya London Marathon London jumapili hii Alphonce Simbu amewasili Uingereza tayari kwa mashindano hayo ambayo yanayotarajiwa kushirikisha wanariadha mashuhuri duniani.
Alphonce, ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon, anatarajiwa kuwapa wakati mgumu manguli wa riadha ulimwenguni wanaoshiriki mbio hizi za London akiwemo Muethiopia Kenenisa Bekele pamoja wa wengine kutoka Ethiopia na Kenya.
|
No comments:
Post a Comment