Wachezaji Marco Reus na Pierre-Emerick Aubameyang na Ousmane Dembele, wameiwezesha timu yao ya Dortmund kutinga hatua ya fainali ya kombe la ujerumani baada ya kuilaza Bayern Munich jumla ya mabao 3-2 ugenini.
Reus ndiye aliyeanza kuifungia bao la kwanza timu yake katika dakika ya 19,kabla ya aubameyang kufunga la pili dakika ya 69 na la tatu lilifungwa na Ousmane Dembele dakika ya 74.
Bayern wenyewe walipata mabao yao kuptia wachezaji wake Javi Martinez dakika ya 28 na Mats Hummels dakika ya 41, mabao ambayo hata hivyo hayakusaidia kwani Dortmund walikaa imara kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
No comments:
Post a Comment