Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya (kulia) akimkabidhi zawadi ya msimu wa Sikukuu ya Chris Mass na Mwaka Mpya kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale katika ofisi za mtandao huo Jijini Dar es Salaam. Zawadi hiyo kutoka kwa kampuni ya Multichoice Tanzania.
Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya na Mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale wakiwa na zawadi hiyo wakati wa kukabidhi.
Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya (kulia) akimkabidhi zawadi ya msimu wa Sikukuu ya Chris Mass na Mwaka Mpya kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale katika ofisi za mtandao huo Jijini Dar es Salaam. Zawadi hiyo kutoka kwa kampuni ya Multichoice Tanzania.
Kampuni ya Multichoice Tanzania wasambazaji wa
visambuzi vya kisasa vya DSTV mapema leo 28 Desemba 2016, wametoa zawadi
ya msimu wa Sikukuu kwa wadau wao mbalimbali ikiwemo kwa mwandishi
Mwandamizi wa mtandao (Blog) wa MODEWJIBLOG, Ndugu Andrew Chale.
Akikabidhi zawadi kwa niaba ya uongozi wa kampuni hiyo ya Multichoice
Tanzania, Costomer Retention Representative, Vida Msuya aliipongeza MO
BLOG na mwanahabari huyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuitangaza
vyema DSTV kwa muda wote na zawadi hiyo ni moja ya kurudisha fadhila kwa
wadau wao.
“Lengo la DST ni kuona tunazidi kuwa na wateja wengi ambao pia wanapata
kitu bora kutoka kwetu. Huduma zetu nzuri na za kisasa hivyo kwa msimu
huu wa Sikukuu wateja wetu na wadau tunawatembea na kuwapatia zawadi.”
Alieleza Vida Msuya.
Aidha, DSTV pia imeweza kuwapatia wadau mbalimbali zawadi hizo za
Sikuukuu na kuwatakia kheri ya Mwaka mpya wa 2017.
Aidha, kupitia kwa Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bw. Alpha
Joseph hivi karibuni amebainisha kuwa katika msimu huu wa kusherehekea
Sikukuu ya krismas na mwaka mpya wateja wao watapata kuangalia chaneli
zaidi ya 70 za DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi
ya Uingereza na zingine nyingi huku wakishusha bei za vifurushi vyao
kwa wastani wa asilimia 16, kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye
chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment