BREAKING
ROSE MHANDO :MSAMA NI BABA KWANGU ACHENI KUNIGOMBISHA NAYE.   UPANDIKIZAJI WA MENO BANDIA KWA NJIA YA KISASA MUHIMBILI MLOGANZILA 45 KUNUFAIKA NA HUDUMA    UTEKAJI WA WATOTO MKUU WA MKOA WA MBEYA JUMA HOMERA AWATAKA WANAFUNZI WA HOLY LAND PRE- & PRIMARY SCHOOL KUKATAA LIFTI   MSAMA ANG'AKA WAIMBAJI WA IN JILI KUPOTOKA MAADILI   DCEA YAFANIKIWA OPERESHENI DAWA ZA KULEVYA YAKAMATA JAHAZI DAWA ZA KULEVYA   NAIBU WAZIRI MKUU AKARIPIA UZEMBE TANESCO   MHE. RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZA NA RAIS WA CHINA MHE. XI JINPING    MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI CHINA..   RAIS SAMIA NCHINI KENYA-ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI   RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA-KENYA    Blogger Tips and Tricks & Blogger Templates

Monday, April 14, 2025

Wednesday, 28 December 2016

YANGA WAITANDIKA NDANDA FC MABAO 4-0

 Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga imeendelea kuwafukuza kwa karibu wapinzania wao wa soka Simba baada ya hii leo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Uhuru Dar es SAlaam

Yanga walianza kuliona lango la Ndanda mapema tu dakika ya nne likifungwa na mshambuliaji wao Donald Ngoma kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kona.

Ndanda wakiwa katika hali ya kuwa na matumaini ya kurejesha bao hilo Yanga walifanikiwa kuongeza bao la pili katika dakika ya 21 likifungwa na Ngoma kwa mara nyingine akiuunganisha krosi safi ya Juma Abdul ambayo ilimparaza beki wa Ndanda na hatimaye kumfikia Ngoma aliyefunga kirahisi.

Ndanda ikiwa bado inajipanga Mshambuliaji Amis Tambwe aliongeza bao la tatu ambapo hadi mapumiko Yanga walikuwa mbele kwa mabao hayo matatu.


Kipindi cha pili Ndanda walizinduka na kujikakamua na kufanya mashambulizi ya kushtukiza lakini ngome ya Yanga ilikuwa imara zaidi, Yanga nayo ilijibu mashambulizi hayo kila wakati, ambapo Yanga walisubiri hadi dakika ya 88, ambapo walipata bao likifungwa na kiungo Vicent Bossou akifunga kwa kichwa,ushindi huo sasa unawaweka nafasi nzuri Yanga kwa kufikisha pointi 40 pointi moja mbele ya wapinzani wao Simba wenye pointi 41,


Vinara wa Ligi hiyo Simba wao wanajitupa Uwanjani kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, kumenyana na Ruvu Shooting.

 


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube