BREAKING

Thursday 11 August 2016

WENGER AJITABIRIA ARSENAL,....

eneja wa klabu ya Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenger amedai kwamba hatma yake katika klabu hiyo ya Emirates inategemea jinsi matokeo ya klabu hiyo msimu huu wa Ligi utakavyokuwa.

Amesema Mkataba wake utakamilika Juni mwakani kwa hivyo anategemea matokeo  ya msimu huu akiamini endapo atafanya vizuri huenda akaongezewa kandarasi nyingine ndani ya klabu hiyo.

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 66, aliajiriwa mwezi Septemba 1996 kuiongoza klabu hiyo, na kuipa mafanikio kadhaa lakini Mkataba wake wa sasa utakamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka ujao.

Arsenal haijashinda taji la ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka wa 2004 jambo ambalo limechochea uhasama dhidi ya Wenger haswa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Awali wenger alikuwa amehusishwa na wadhifa wa kocha wa timu ya Uingereza lakini Sam Allardyce akachaguliwa kuchukua nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube