Kampuni ya Multchoice Tanzania leo imezindua rasmi msimu wa English Premier League ambayo inaanza rasmi Agosti 13.
Wakati wa uzinduzi huo kupitia DStv, Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania, Maharage Chande amesema mechi 300 kati ya 380 zitaonyeshwa Live.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo, Maharage amesema pamoja na kuongeza mechi za Live, Watanzania hadi wenye king’amuzi cha Sh 23,000 nao wataona Live mechi za Premier League ambayo ni mechi maarufu zaidi ya soka duniani.
“Hii ni asilimia 80 ya mechi za Ligi Kuu England ambacho ni kitu kikubwa. Hakuna king’amuzi kingine kitaonyesha mechi nyingi live kama chetu,” alisema Maharage.
Pamoja na Premier League, wataonyesha moja kwa moja mechi nyingi za La Liga.
Ving'amuzi vya DStv ndiyo vikongwe kabisa hapa nchini katika uonyesha wa malipo na ndiyo vinavyoonyesha Ligi Luu England, La Liga, Bundesliga na michuano mingine mikubwa ya soka.
No comments:
Post a Comment