BREAKING

Tuesday, 23 August 2016

KIJANA ALIYEENDA KUSOMA UJERUMANI, AITUMIA FURSA HIYO KUSAKA WAWEKEZAJI NCHINI

*NI PETRO MAGOTI
*AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BILLIONEA KNOOP, NCHINI HUMO

Kijana Petro Magoti kutoka Shirikisho la Vyuo
vya Elimu ya Juu-CCM,  aliyeko Ujerumani kwa
 masomo ya Uongozi na Uhusiano wa Kimataifa,
 akiagana na mmoja wa wamiliki wa viwanda
vikubwa Duniani, Prof. Karl Knoop, baada ya
kuzungumza naye,  mjini Berlin, Ujerumani, juzi.
Kushoto ni Meya  wa mji wa Bugermeister,
 David Osthotlhoff.
NA BASHIR NKOROMO
Katika kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifikisha Tanzania katika mapinduzi ya viwanda vikubwa na Vidogo, Kijana Petro Magoti ambaye ni mwakilishi pekee kwa Tanzania aliyeko nchini Ujerumani, kwenye mafunzo ya uongozi na uhusiano wa kimataifa, amekutana na mmoja wa wamiliki wa viwanda vikubwa Duniani, Prof. Karl Heinz Knoop na kufanya mazungumzo naye ili kumshawishi kuja kuwekeza nchini.

Akizungumza kutoka nchini Ujerumani, Magoti amesema leo kwamba, Prof. Knoop ambaye anamiliki viwanda katika nchi 17 Barani Ulaya na katika nchi nne katika bara la Afrika, katika mazungumzo yao, Prof. Knoop ameonyesha dhamira ya kuwekeza Tanzania katika meneo ya Himo mkoani Kilimanjaro na Kilindi mkoani Tanga.


Magoti amesema, Prof, Knoop, amefikia dhamira hiyo baada ya kumweleza kwa kina fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania, na namna nchi ilivyojipanga kuwapokea kwa ukarimu wawekezaji kutoka nchi za nje ikiwemo Ujerumani, lengo likiwa kuifikisha nchi kuwa yenye viwanda na hivyo kuwezesha wananchi wengi wakiwemo vijana kupata ajira za uhakika.


"Katika mazungumzo yetu, Prof. Karl Heinz Knoop ameeleza kuwa na dhamira ya kuwekeza Tanzania ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuondoa umasikini, hata hivyo akasema, awali amewahi kuonyesha azma hiyo kwa wakati, lakini akakumbana na changamoto lukuki ikiwemo kupewa eneo la kujenga viwanda vikubwa vya mashine za kilimo kama vile Matrektar, Mashine za kupanda mbegu, Kuvuna na kukausha mazao, na Maghala makubwa ya kuhifadhia vyakula na kiwanda cha magari makubwa ya mizigo", aalisema Petro.


Alisema,  katika mazungumzo yao, alimsihi na kumwomba Billionea huyo, Prof. Knoop, kutokata tamaa katika dhamira yake hiyo ya kujenga viwanda Tanzania kutokana changamoto ya awali aliykumbana nayo ya kupata eneo la uwekezaji, badala yake afike Tanzania ili kuonana na Rais John Magufuli ambaye kwake viwanda ni kipaumbele kikubwa.


"Nilimweleza kuwa Mh. Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli, anavutiwa saa na wawekezaji walio tayari kuijenga Tanzania ya viwanda ili kukuza Uchumi na kupunguza tatizo la ajira hasa kwa Vijana ambalo sasa ni kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali, lakini nikamshauri pia Billionea huyo kuwa akifika nchini kwetu, aombe kujenga viwanda vyake katika mikoa ya Iringa na Morogoro ambayo kwa kuwa mikoa hiyo ina maeneo mengi na mazuri kwa Kilimo.", Magoti alisema Magoti na kuongeza,


"Baada ya mazungumzo yetu tumekubaliana kwamba kati ya tarehe 17 hadi 22 Oktoba, mwaka huu, Bilionea huyo atafika Tanzania kwa ajili ya kuonana na Mh. Rais ili kujadiliana nae juu ya uwekezaji huo wa viwanda na ameahidi kutembelea mikoa ya Iringa na Morogoro ili kujiridhisha na maeneo yalivyo kwa ajili ya Uwekezaji katika Viwanda vya Kilimo.


Katika kuhakikisha kuwa fursa ya yeye kuwa nchini Ujerumani, anaitumia vilivyo kwa manufaa ya taifa, Magoti alitafuta nafasi na hatimaye akaipata ya kukutana na Wabunge wastaafu na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Ujerumani wakiongozwa na Prof. Hemker anaetokana na Chama cha SPD.


Katika yake na viongozi hao kutoka Kada mbali mbali Nchini Ujerumani wengi wao wamekubali na kuahidi kuwa wako tayari kumuunga mkono Rais wa Dk. John Magufuli katika azma yake ya kuijenga Tanzania yenye viwanda vingi, na hivyo wameahidi kuja Tanzania kujenga viwanda vya kutengeneza mashine za aina mbalimbali hususan za kilimo.


Magoti ambaye anatoka katika Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, hupo Berlin, nchini Ujerumani kwa wiki ya pili sasa, akiendelea na  masomo ya Uongozi na Uhusiano wa Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube