- Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Mh. Husein Bashe akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla. (kushoto). Wabunge hao walikuwa ndiyo wenyeji katika ugeni huo mkubwa kutokana na Rais kufanya mkutano ndani ya majimbo yao hayo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla wakati Mh. Rais Magufuli alipowasili katika makazi ya Rais mjini Nzega akitokea Mkoa wa Singida alipoanzia ziara yake hiyo.
Bishop Chakupewa wa Nzega akitoa neno la Mungu wakati wa Mkutano huo wa Rais Magufuli alipotembelea Nzega, Mkoani Tabora. katika mkutano wa kushukuru Julai 30.
Askofu Mzoka kutoka kanisa la Romani Cathoriki Nzega
Mbunge wa Nzega Mjini, Mh. Hussein Bashe akitoa neno kwa wananchi wakati wa mkutano huo
Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli akisalimia wanannchi.
Wananchi waliofurika wakishangilia wakati Rais Magufuli akipanda jukwaani
Rais Magufuli akihutubia jukwaani.
Sehemu ya umati wa tukio hilo..
Rais Magufuli akitoa salamu kwa wananchi wa Nzega wakati wa kuelekea kupanda jukwaani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli apongeza na
kufurahishwa na juhudi za Wabunge Vijana wanaoongoza Majimbo ya Nzega
Mjini ambalo linaongozwa na Mbunge Husein Bashe na lile la Nzega
Vijijini linaloongozwa na Mbunge ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla.
ambapo amewahakikishia kutatua kero zao kubwa ya maji ambayo
inawakabili wananchi wengi katika Majimbo hayo.
Rais
Dk. Magufuli ambaye aliweza kufanya mkutano mkubwa wa wazi ndani ya
viwanja vya Nzega mjini, Julai 30, alibainisha kuwa, anafahamu matatizo
wanayokabiliana nayo Wananchi wa majimbo hayo likiwemo suala hilo la
maji ambapo amewaambia wamwachie alifanye kazi hilo huku suala lao la
kutaka Mkoa mpya lisubiri kwanza mpaka atakapomaliza kero muhimu kwa
wananchi ikiwemo kuwapatia huduma bora za afya, Madawa .
“Tatizo
la Maji katika Wilaya Nzega ninalipokea na nitalifanyia kazi. Tanzania
imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India.
Fedha ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa
Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge na Uyui pamoja
na vijiji vilivyopo kandokando mwa bomba kuu kuanzia mwaka huu ambapo
watu milioni moja na laki moja (1,100,000)watanufaika.” Alieleza Rais
Magufuli.
Rais
Magufuli ameongeza kuwa, Serikali imefanya usanifu na upembuzi
yakinifu kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya kutoka mto
Malagarasi kwa ajili ya Miji ya Urambo, Kaliua na Nguruka pamoja na
vijiji vilivyopo kandokando mwa bomba kuu ambako watu laki sita
(600,000) watanufaika hivyo katika tatizo la maji wananchi wa maeneo
hayo wataondolewa kero yao kubwa ya maji.
Aidha, Rais Magufuli amepiga marufuku wakulima wadogo kutozwa ushuru wa mazao watokapo na mazao mashambani.
"Ninapenda
tukusanye kodi, lakini sio kukusanya kodi kutoka kwa watu masikini, mtu
ametoka shambani na magunia yake mawili au hata matano halafu nyinyi
mnamtoza kodi.
"Mimi sipendi kuwanyanyasa hawa watu wanyonge, mtu akiwa na mazao lori
zima hapo sawa lakini sio kwa mtu mnyonge mwenye gunia moja" Amesema
Rais Magufuli wakati wa kutoa taarifa maalum ya kuzuia watu
wanaonyanyasa wakulima wadogowadogo pamoja na wananchi katika suala la
kuwakusanyia ushuru.
No comments:
Post a Comment