Shirikisho la soka Tanzania TFF limethibitisha kuwa beki mpya wa Yanga, Hassan Ramadhani Kessy atacheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu mpya ambao Ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi kesho.
Akizungumza na channel ten Afisa Habari wa TFF Alfredy Lucas amesema Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyoketi jana chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Richard Sinamtwa imemtaka beki huyo kuilipa klabu ya zamani, Simba kwa kuvunja Mkataba.
Lucas amesem kuwa Kamati imejiridhisha kwamba Kessy alivunja Mkataba na Simba kinyume cha utaratibu hivyo anapaswa kuilipa Simba.
Kessy alisajiliwa na Simba misimu miwili iliyopita kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa Mkataba wa miaka miwili akilipwa
No comments:
Post a Comment