Mo amesema ameandika barua hiyo leo asubuhi baada ya kusikia baadhi ya viongozi wa Simba wakisema hakuwa amefanya hivyo,ambapo amesema alichokiandika ndani ya barua hiyo ni kuueleza uongozi huo kutoa ofa ya Sh bilioni 20 ili kupata hisa asilimia 51, huku akikanusha kauli za uongozi huo katika mktano wa jana kwamba hajawahi kukutana na viongozi hao ambapo amesema amewahi kukutana na Rais wa Simba, Evans Aveva zaidi ya mara tatu.
Mo amesema katika barua hiyo ameandika mambo mbali mbali ikiwepo kueleza kuwa ni mwanachama aliyewahi kuwa mfadhili wa timu, ambaye sasa anataka awekeze Sh. Bilioni 20 kwa kununua asilimia 51 ya hisa za klabu.
Baada ya kufanya mkutano huo na waandishi wa habari muda mfupi Mo alipokea barua kutoka Uongozi wa Simba kujadiliana naye juu ya mpango wa kununua hisa za klabu hiyo.
Katika barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa klabu, Patrick Kahemele leo uongozi wa Simba umemuomba Mo Dewji kuhudhuria kikao cha Kamati ya Utendaji Agosti 15, mwaka huu.
Katika barua hiyo imeeleza kikao hicho kifanyike Agosti 15 kwa sababu wiki hii watakuwa wametingwa na shughuli za wiki ya Simba kuelekea tamasha la Simba Day Agosti 8, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment