BREAKING

Monday, 29 August 2016

DC MTATURU AWATAKA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA HIFADHI KUHAMA NDANI YA MWEZI MMOJA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa taarifa juu ya kusimama kwa ujenzi wa Zahanati hiyo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri wakati akitoa maelezo wakati wa kikao cha serikali ya kijiji

Tuesday, 23 August 2016

KIJANA ALIYEENDA KUSOMA UJERUMANI, AITUMIA FURSA HIYO KUSAKA WAWEKEZAJI NCHINI

*NI PETRO MAGOTI
*AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BILLIONEA KNOOP, NCHINI HUMO

Kijana Petro Magoti kutoka Shirikisho la Vyuo
vya Elimu ya Juu-CCM,  aliyeko Ujerumani kwa
 masomo ya Uongozi na Uhusiano wa Kimataifa,
 akiagana na mmoja wa wamiliki wa viwanda
vikubwa Duniani, Prof. Karl Knoop, baada ya
kuzungumza naye,  mjini Berlin, Ujerumani, juzi.
Kushoto ni Meya  wa mji wa Bugermeister,
 David Osthotlhoff.
NA BASHIR NKOROMO
Katika kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifikisha Tanzania katika mapinduzi ya viwanda vikubwa na Vidogo, Kijana Petro Magoti ambaye ni mwakilishi pekee kwa Tanzania aliyeko nchini Ujerumani, kwenye mafunzo ya uongozi na uhusiano wa kimataifa, amekutana na mmoja wa wamiliki wa viwanda vikubwa Duniani, Prof. Karl Heinz Knoop na kufanya mazungumzo naye ili kumshawishi kuja kuwekeza nchini.

Akizungumza kutoka nchini Ujerumani, Magoti amesema leo kwamba, Prof. Knoop ambaye anamiliki viwanda katika nchi 17 Barani Ulaya na katika nchi nne katika bara la Afrika, katika mazungumzo yao, Prof. Knoop ameonyesha dhamira ya kuwekeza Tanzania katika meneo ya Himo mkoani Kilimanjaro na Kilindi mkoani Tanga.


Magoti amesema, Prof, Knoop, amefikia dhamira hiyo baada ya kumweleza kwa kina fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania, na namna nchi ilivyojipanga kuwapokea kwa ukarimu wawekezaji kutoka nchi za nje ikiwemo Ujerumani, lengo likiwa kuifikisha nchi kuwa yenye viwanda na hivyo kuwezesha wananchi wengi wakiwemo vijana kupata ajira za uhakika.


"Katika mazungumzo yetu, Prof. Karl Heinz Knoop ameeleza kuwa na dhamira ya kuwekeza Tanzania ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuondoa umasikini, hata hivyo akasema, awali amewahi kuonyesha azma hiyo kwa wakati, lakini akakumbana na changamoto lukuki ikiwemo kupewa eneo la kujenga viwanda vikubwa vya mashine za kilimo kama vile Matrektar, Mashine za kupanda mbegu, Kuvuna na kukausha mazao, na Maghala makubwa ya kuhifadhia vyakula na kiwanda cha magari makubwa ya mizigo", aalisema Petro.


Alisema,  katika mazungumzo yao, alimsihi na kumwomba Billionea huyo, Prof. Knoop, kutokata tamaa katika dhamira yake hiyo ya kujenga viwanda Tanzania kutokana changamoto ya awali aliykumbana nayo ya kupata eneo la uwekezaji, badala yake afike Tanzania ili kuonana na Rais John Magufuli ambaye kwake viwanda ni kipaumbele kikubwa.


"Nilimweleza kuwa Mh. Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli, anavutiwa saa na wawekezaji walio tayari kuijenga Tanzania ya viwanda ili kukuza Uchumi na kupunguza tatizo la ajira hasa kwa Vijana ambalo sasa ni kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali, lakini nikamshauri pia Billionea huyo kuwa akifika nchini kwetu, aombe kujenga viwanda vyake katika mikoa ya Iringa na Morogoro ambayo kwa kuwa mikoa hiyo ina maeneo mengi na mazuri kwa Kilimo.", Magoti alisema Magoti na kuongeza,


"Baada ya mazungumzo yetu tumekubaliana kwamba kati ya tarehe 17 hadi 22 Oktoba, mwaka huu, Bilionea huyo atafika Tanzania kwa ajili ya kuonana na Mh. Rais ili kujadiliana nae juu ya uwekezaji huo wa viwanda na ameahidi kutembelea mikoa ya Iringa na Morogoro ili kujiridhisha na maeneo yalivyo kwa ajili ya Uwekezaji katika Viwanda vya Kilimo.


Katika kuhakikisha kuwa fursa ya yeye kuwa nchini Ujerumani, anaitumia vilivyo kwa manufaa ya taifa, Magoti alitafuta nafasi na hatimaye akaipata ya kukutana na Wabunge wastaafu na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Ujerumani wakiongozwa na Prof. Hemker anaetokana na Chama cha SPD.


Katika yake na viongozi hao kutoka Kada mbali mbali Nchini Ujerumani wengi wao wamekubali na kuahidi kuwa wako tayari kumuunga mkono Rais wa Dk. John Magufuli katika azma yake ya kuijenga Tanzania yenye viwanda vingi, na hivyo wameahidi kuja Tanzania kujenga viwanda vya kutengeneza mashine za aina mbalimbali hususan za kilimo.


Magoti ambaye anatoka katika Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, hupo Berlin, nchini Ujerumani kwa wiki ya pili sasa, akiendelea na  masomo ya Uongozi na Uhusiano wa Kimataifa.

Friday, 19 August 2016

HASSAN KESSY HURU KUCHEZEA YANGA LIGI KUU BARA


Shirikisho la soka Tanzania TFF limethibitisha kuwa beki mpya wa Yanga, Hassan Ramadhani Kessy atacheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu mpya ambao Ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi kesho.

Akizungumza na channel ten Afisa Habari wa TFF Alfredy Lucas amesema Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyoketi jana chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Richard Sinamtwa imemtaka beki huyo kuilipa klabu ya zamani, Simba kwa kuvunja Mkataba.

Lucas amesem kuwa  Kamati imejiridhisha kwamba Kessy alivunja Mkataba na Simba kinyume cha utaratibu hivyo anapaswa kuilipa Simba.

Kessy alisajiliwa na Simba misimu miwili iliyopita kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa Mkataba wa miaka miwili akilipwa 


LIGI KUU TANZANIA B ARA SIMBA KUWAVAA NDANDA FC KESHO







Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kwa viwanja vitano kuwaka moto huku mchezo wa kusisimua ukizikutanisha timu ya Simba na Ndanda FC wanakuchele kutoka Mtwara kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Tanzania Boniface Wambura amesema kuwa maandalizi yake yamekmilika na sasa ni soka kupigwa viwanjani.

Wakati huo huo Wambura amezungumzia utatuzi wa changamoto ya Ligi wakileta mabadiliko kadhaa toifauti na msimu ulioptya ikiwepo kurekebisha ratiba pamoja na kuzingatia kuanza mapema kwa ligi hiyo.


MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WATENGENEZA AJIRA KWA WAJASILIAMALI VIJIJINI KUPITIA MRADI WA MADAWATI

 Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia)  na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale.
Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang'wale.
Utengenezaji wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano.
Fursa ya ajira iliendelea kusambaa kwa dereva wa trekta Bw ,Machibya aliyepata tenda ya kusafirisha Madawati kwenda katika shule zilizokusudiwa kupata Madawati hayo.
Lakini pia wakati wa shughuli za utengezaji wa Madawati hayo mafundi walihitaji kupata chakula na hii pia ikawa Fursa kwa Mama Nitilie Devotha Sonda wa Sonda ambaye alikuwa akitoa huduma ya chakula kwa mafundi hao.



Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
 
Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umetengeneza mamia ya ajira kwa vijana na wanawake wanaoishi maeneo mbalimbali mkoani shinyanga na Geita kupitia mpango wa kutengeneza madawati elfu sita katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 200.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana wamesema neema ya kujiingizia vipato kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali katika zoezi la kutengeneza madawati imebadili maisha yao hasa katika msimu huu wa kiangazi ambao wengi wao ajira zao zimesimama kwani walio wengi wanategemea mvua kwenye ajira yao ya msingi ya kilimo.

“Tunashukuru sana msimu huu wa kiangazi, tumepata nafasi ya kupata kazi za ambazo zinatupatia kipato kupitia utengenezaji wa madawati, mimi hapa ni fundi chuma, nachomelea vyuma na kazi yangu hii huku vijijini wateja ni wachache sana, muda mwingi huwa tuko doro kwenye kijiwe chetu lakini sasa hivi tuna kazi nyingi sana za kutengeneza madawati hapa imebidi niajiri vijana wengine watano kuweza kunisaidia kukamilisha kazi ya kuunganisha vyuma kwa ajili ya madawati mia tano ambayo tumepata tenda na Kampuni iliyoshinda tenda ya kutengeneza madawati kwa gharama ya mgodi wa dhahabu ya Bulyanhulu.” Anasema Abbas Mbua mkazi wa kata ya Msalala wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.

“Sisi wapiga msasa tunajipatia shilingi elfu kumi na tano kwa kila dawati 5 hii si haba, kiasi hiki kimenisaidia sana maana sikupata vizuri mazao mwaka huu kwa hiyo pesa niliyoingiza kwenye kazi ya kupiga msasa imebadili kabisa hali halisi nyumbani, nimenunua gunia za mahindi, maharage na mchele, hali imetulia kwa kweli siwezi kusema uongo” anasema Maige Deus mkazi wa Kahama.

“Ninaiomba sana serikali yetu iendelee kuvumbua miradi mingine ili sisi vijana tuendelee kuchapa kazi, maana vinginevyo tunakaa vijiweni kazi hamna, lakini mradi huu wa madawati ulivyokuja hatuna hata muda wa kuvuta sigara, tuko bize kutwa nzima tunatengeneza madawati, hapa mimi ndiyo fundi mkuu kwenye hiki kiwanda naunganisha mbao na kuhakikisha madawati yako vizuri kwa ajili ya wanafunzi.” Anasema Abdul Karim Ramadhani akiwa katika kiwanda cha Zacharia and Deus Timber Supply cha Nyang’wale mkoani Geita.

Halikadharika mama nilitie nao wanasema si haba mradi wa kuchonga madawati umeongeza idadi ya wateja katika migahawa yao, Devotha Sonda wa Sonda Mama Nitiliea katika kijiji cha Msalala anasema “ Kabla ya mradi wa madawati vyakula hapa tulikwa tunapika kidogo na wateja walikuwa ni wa kubangaiza tu lakini sasa hivi kutokana uchongaji wa madawati vijana ni wengi sana na binafsi nimepewa tenda kabisa ya kupikia vijana wanaotengeneza madwati na ninalipwa vizuri na kwa muda, naomba miradi kama hii iendelee tu hadi madawati yatoshe na sisi mitaji itakuwa imekua. Mwaka huu maswala ya ada kwa watoto, mavazi sasa ni jambo rahisi.”

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya kizawa ya Zacharia and Deus Timber Supply Deus Mlela iliyopo Nyang’wale kilomita hamsini kutoka mgodi wa Bulyanhulu amesema, “Tenda ya kutengeneza madawati mia tano kutoka Bulyanhulu kwetu tumepata faida mara mbili kwanza imetuongezea mtaji na pili imetupa uwezo na kujulikana kwa wadau wengine, sasa hivi tumepatiwa tena tenda na Halamashauri ya wilaya kutengeneza madawati mengine elfu moja na kampuni nyingine imetupa tenda na madawati mia mbili, bila kazi ya Bulyanhulu kutufungulia mlango ingekuwa vigumu kuweza kupokea tenda hizo kwa sababu mtaji ulikuwa mdogo. Tunaomba wadau waendelee kutuamini ili na sie tuweze kuendelea kusambaza ajira kwa vijana ambao hawana ajira.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama amesema, “Kimsingi kuwa karibu na Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu imewafanya watu wa Nyang’wale ule uzito wa kazi ya madawati kuwa tofauti na sehemu nyingine, japo hatujamaliza kabisa tuna mapungufu kidogo, faida ya mradi wa madati faida yake ya kwanza ni kwa watoto wa shule ambayo ni walengwa, wanapata madawati wake vizuri na waweze kuelewa masomo yao vizuri,  kwa njia nyingine mpango huu umetengeneza ajira, wale watengeneza mawadaati wamepata kazi ya kufanya na kipato, wanajipatia mahitaji wengine wananunua mifugo, kwa mfano katika mradi huu bulyanhulu imedhamini madawati yenye thamani ya shilingi million thethini na tano na hii pesa imezunguka kwa watu wote, mafundi seremala, waendesha mikokoteni, mama nitilie, na wengine wengi wamejipatia kipato na hata mitaji.”

Mwaka 2013 Mgodi wa Bulyanhulu ulitoa madawati 1329 kwa ajili ya shule 10 za msingi  zinazozunguka mgodi  wa Bulyahulu.

Mwaka huu 2016 Madawati 1380 kwa halmashauri ya Msalala madawati  500 kwa wilaya ya Nyang’wale 500, madawati 2000 yatatolewa hivi karibuni kwa mkoa wa Shinyanga na pia Bulyanhulu itaipatia dola za kimarekani elfu 6000 shule ya msingi ya binafsi ya St. Josephine Bhakita iliyoko km 12 kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika kijiji cha Ilogi kata ya Bulyanhulu.

BENKI YA DUNIA KUENDELEA KUISAIDIA SEKTA YA MAJI NCHINI

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua  kikao cha pamoja na ujumbe wa Benki ya dunia, Wizara ya Maji ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco ) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa) namna ya kutatua changamoto za usambaza Maji kwenye Jiji la Dar es Salaam yakiwamo Mivujo na Miundombinu chavu , kilichofanyika Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam.
KATIKA kuhakikisha sekta ya Maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya huduma ya maji, Benki ya Dunia imejitolea kulisaidia Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Majitaka katika maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird, ambaye alikuwa ameambatana na wajumbe wake katika kikao cha pamoja na Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, pamoja na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO). 

Kikao ambacho kililenga uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.

Aidha, Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia, ameridhishwa na juhudi za makusudi zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi, pamoja na kupambana na kiwango cha Maji kinachopotea bila sababu ya msingi. 

Ameeleza kuwa Benki ya dunia imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Majisafi na Majitaka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” ili kuwapunguzia akina mama wengi tatizo la Maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa wahanga wakuu wa tatizo hilo.

Nimeridhishwa na utendaji wenu wa kazi, jinsi ambavyo mmejipanga katika kufanya kazi, hasa juhudi zenu mnazoziweka katika kupambana na upotevu wa Maji na kuwapatia wananchi huduma ya Maji alisema Bi. Bird

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha kilichotengwa na Benki ya Dunia kitatumika katika kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya Maji.

Saturday, 13 August 2016

TANZANIA KUTUMIA DOLA MIL500 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba  akifungua warsha ya wadau wa kuhusu ripoti ya taarufa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
 Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani Tanga.


 Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa Tanzania katika Juhudi za Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi  kushoto ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani  Richard Muyungi
TANZANIA inatarajiwa kutumia takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka 2030 ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchi.

Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza  juhudi za kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aliitaja baadhi ya miradi ambayo itatekelezwa ili kupunguza gesi joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni katika Jiji la Dar Es Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya Mbinga,Makete,Njombe Usa River na Ifakara.

“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati tano(5MW) za uzalishaji wa hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka hazitaweza kuchukuliwa athari za kimazingira zinaweza kuendelea kujitokeza”alisema Waziri Makamba.

Ambapo alisema katika kushiriki  juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi joto tayari serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa fursa kwa wadau ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi .

Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa sasa imeshaanza kutekelezwa katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na Halimashauri mbalimbali hapa nchini.

“Juhudi za serikali ni kuhimiza matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa nishati ya umeme yanaongezeka ili kuweza kupunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa ukaa ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza Waziri Makamba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani  Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali nchini.

Alisema ilikuweza kuwa na mipango madhubuti katika utekelezaji mkakati wa taifa wa mawasilinao wa mabadiliko ya tabia nchi kupitia wizara za kisekta.

Friday, 12 August 2016

MWENYEKITI WA CCM, RAIS DK. MAGUFULI ARIPOTI RASMI, OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Johnn Magufuli akipokewa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika katika ofisi hiyo, akiwa Mwenyekiti wa Chama. Kulia ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akimsalimia Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Abdallah Bulenbo,alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akimsalimia Angela Kairuki alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiendelea kuwasalimia wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
  
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisaini kitabu baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), kumuonyesha Ofisi yake Mwenyekiti huyo, alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Wazir Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia na Mweyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiendelea kusaini vitabu Ofisini kwake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akitoa maneno ya kumkaribisha rasmi kwenye Ofisi yeke ya Uenyekiti wa CCM, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli
 Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akishukuru baada ya kusaini Vitabu na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kumuonyesha rasmi ofisi. 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mama Janneth Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwa mezakuu na viongozi waandamizi alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akimkaribisha Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye kumkariisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, ili kuendelea na shughuli 
 Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akizungumzabaada ya kupewa nafasi na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye
 Wananchi wakishangilia kwa bashasha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akizungumza kama Mwenyeji wa mapaokezi ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk, John Magufuli
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akimkaribisha Kinana kumkariisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli kuzungumza na wana CCM na wananchi, Nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Dar es Salaam, leo
 Katibu Mkuu akimkaribisha Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa kabla ya kumkaribisha Dk. Magufuli
 Waziri Mkuu Majaliwa Kaasim Majaliwa akizungumza kabla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kupanda jukwaani.
 Wananchi wakishangilia
 Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia, akizungumza baada ya kukaribishwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli kusalimia hadhara. Zifuatazo ni Picha zinazoonyesha Dk. Magufuli akionyesha msisitizo  wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM.



 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM waliomlaki kwa shauku alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Watu wa kila rika walimsikiliza Dk. Magufuli kwa makini sana
Baadaye Dk. Magufuli alipanda jukwaa la Kikundi cha TOT na kucharaza tumba, kuonyesha umahiri wake pia  katika fani ya burudani.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube