BREAKING

Thursday, 5 May 2016

SNURA AKUBALI YAISHE,AJITETEA KUFUNGIWA WIMBO WAKE..

Mwimbaji wa nyimbo za Mduara nchini Snura Mushi ameomba radhi kwa umma wa Watanzania kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mitandaoni, video ambayo imefungiwa jana na Serikali kupitia Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na Michezo kutokana na ukiukwaji wa maadili ndani ya wimbo huo na video yake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam Snura ameomba radhi kwa mashabiki wake na watanzania wote akisema wakati wa utayarishaji wa video hiyo hakutambua kama ingepokewa tofauti, hivyo atafanya jitihada za kuhakikisha anauboresha zaidi.

Naye meneja wake alizungumzia utetezi huo akiomba watanzania kuwasamehe yeye pamoja na msanii huyo, kwani sasa wamejifunza ikiwepo kupata usajili wa BASATA utakaomwezesha kufanya kazi zake kwa huru.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube