Mwamuzi
Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam, Jumatano Mei 25, 2016 ameteuliwa
kuwa mwamuzi atakayechezesha mchezo wa fainali za Kombe la Shirikisho
maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayozikutanisha timu
za Young Africans na Azam FC; zote za jijini Dar es Salaam.
Mchezo
huo utakaoanza kesho saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam waamuzi wasaidizi watakuwa Ferdinand Chancha wa Mwanza (line 1)
na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es Salaam (line 2) na mwamuzi wa
akiba mezani ni Frank Komba wa Dar es Salaam pia. Kamishna wa mchezo huo
anatakuwa Juma Mgunda wa Tanga.
Kwa
mujibu wa kanuni za Ligi Kuu msimu 2015/16, mabingwa wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu 2015/16 wataiwakilisha nchi katika michuano
ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2016/17. Nafasi hiyo imechukuliwa na
Young Africans.
Kadhalika
Azam ina tiketi tayari ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika
kwa kufika fainali za ASFC ingawa kanuni zinataka bingwa ambako kwa
upande wa Yanga wana tiketi ya michuano ya juu zaidi ya shirikisho.
Mvuto wa mchezo wa Jumatano ni ushindani wa soka na zawadi kwa bingwa.
Fainali
za Kombe la Shirikisho zinakuja baada ya mchuano ulioshindanisha timu
64 za Ligi Kuu Tanzania Bara - VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL
(24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24).
No comments:
Post a Comment