BREAKING

Monday 23 May 2016

ENGLAND YAITANDIKA UTURUKI

Timu ya soka ya Taifa ya England imeanza maandalizi ya fainali za Mataifa ya Ulaya, 2016 kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Uturuki.
Ushindi huo ulipatikana katika katika Mechi ya kirafiki iliyopigwa katika Uwanja wa Etihad Jijini Manchester kupitia wachezaji Harry Kane anayeichezea Tottenham na Jamie Vardy wa Leicester City.
England walifunga Bao lao Dakika ya 3 kupitia Harry Kane na Turkey kusawazisha Dakika ya 13 kwa Bao la Hakan Calhanoglu.
Kipindi cha Pili Dakika ya 71 England walipata Penati baada ya Jamie Vardy kuangushwa na Topal lakini Harry Kane alikosa Penati hiyo kwa kupiga nje.
Dakika ya 83 Jamie Vardy aliipa England Bao lao la pili kufuatia Kona ambapo Gary Cahill alipiga Kichwa Golini na Kipa wa Turkey Babacan kugongana na Beki wake na kutoa mwanya kwa Vardy kufunga.
Katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa Marekani imefanikiwa kuichapa Puerto Rico mabao 3-1.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube