BREAKING

Tuesday 24 May 2016

WAZIRI NAPE AWAKUMBUSHA WANAMICHEZO NCHINI KUZINGATIA SUALA LA NIDHAMU NDANI NA NJE YA UWANJA ILI KUONGEZA UFANISI

   Baadhi ya wanamichezo wa kutoka Vikundi mbalimbali vya Jeshi wakiwa Jukwaani wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.
Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye, amezindua mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ,CDF katika

Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, huku akiwakumbusha wanamichezo wanaoshiriki mashindano hayo suala zima la nidhamu michezoni..

Waziri Nape Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa mashindano ambayo pia ni maandalizi ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya Afrika Mashariki nchini Rwanda ambapo amevipongeza vikosi mbalimbali vya timu za majeshi kwa kuliletea sifa taifa mara zote.

Naye Kaimu Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ,Meja Generali Simon Mumwi, akizungumzia mashindano hayo amepongeza mwitikio wa wanamichezo pamoja na kumuahidi waziri Nape kuwa timu za Tanzania zitarejea na ushindi katika Mashindano ya Rwanda.

Awali vikundi mbalimbali vya burudani vilifanya maonyesho, mbalimbali ikiwepo ngoma, bendi za muziki , ambapo baadae Waziri Nape alifungua rasmi mashindano hayo kwa mchezo wa soka kati ya timu ya JKT na Tembo 


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube