KIKOSI CHA YANGA
WACHEZAJI WA TP MAZEMBE
Timu ya Yanga imepangwa kundi la A katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mabingw wa zamani barani,Afrika TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Kundi B linaundwa na timu za Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za Morocco.
Ratiba hiyo inamaanisha Yanga itakutana na timu ya mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC, katika mchezo wa awali.
Katika Ligi ya Mabingwa Afrika kundi A kuna timu za Zesco United ya Zambia, Al Ahly ya Misri, Asec Mimosa ya Ivory Coast, Waydad Casablanca ya Morocco, wakati Kundi B kuna Enyimba ya Nigeria, Zamalek ya Misri, ES Setif ya Algeria na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment